JK, MAMA SALMA KATIKA MKUTANO WA JUMUIYA YA MADOLA
Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mwenyekiti wa watanzania waishio
Australia, Asimwe Kabunga katika mkutano unaowajumuisha watanzania
waishio Australia. Rais Kikwete pamoja wanajumuia ya watanzania
wanaoishi Australia wamezungumzia masuala mbalimbali ya maendeleo.
(PICHA ZOTE NA MWANAKOMBO JUMAA-MAELEZO) Baadhi ya wanajumuia wanaoishi nchini Australia wakimsikiliza Rais Jakaya Kikwete (hayupo pichani) alipokutana nao nchini Perth. Mke
wa Rais, Mama Salma Kikwete akibadilisha mawazo na mwanajumuia wa
kitanzania aishie Australia, Dk. Joseph Masika wakati Rais Jakaya
Kikwete alipokutana na wanajumuia hao wanaoishi Australia na kuzungumza
nao mambo mbalimbali ya maendeleo ya nchi yetu.
Mke
wa Rais, Mama Salma Kikwete (kulia) akipokea maua kutoka kwa mweka
Hazina wa Jumuia ya Watanzania waishio Australia, Maryam Powell,
walipokutana na wanajumuia mjini Perth Australia. Rais Jakaya Kikwete
alikutana na wanajumuia kuzungumza mambo mbalimbali ya maendeleo na
kijamii. Rais yupo nchini Australia kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi
wanachama wa Jumuia ya Madola. Wanajumuia
wa kike wanaoishi Australia wakiwa katika picha ya pamoja na Mke wa
Rais, Mama Salma Kikwete baada ya kumalizika mkutano wa Rais Kikwete na
Watanzania wanaoishi Australia jana.
No comments:
Post a Comment