KESI YA EPPA YASIKIKA KIZIMBANI

....FARIJALA HUSSEIN NA RAJAB MARANDA....
Hukumu
ya kesi ya wizi wa Sh bilioni 1.8 katika Akaunti ya madeni ya nje (EPA)
ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetolewa leo kwa
Farijala Hussein na ndugu yake Rajabu Maranda,wamehukumiwa kifungo
cha miaka mitano jela ambapo pia wametakiwa kurudisha fedha hizo kwa
Serikali
Jopo la majaji watatu likiongozwa na Mh Saul Kinemela,limewatia hatiani
kwa mashitaka nane yanayowakabili shitaka la kwanza lilifutwa kwa kuwa
upande wa mashitaka ulishindwa kuthibitisha hilo,Kwa kosa la pili
mshitakiwa wa kwanza pekee atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela,kosa
la tatu na la nne
washitakiwa wote watatumikia adhabu ya miaka mitano,kosa la tano
mshitakiwa wa pili pekee atatumikia adhabu ya miaka miwili jela huku
Kosa la sita washitakiwa wote kwa pamoja watatumikia adhabu ya miaka
miwili jela na kosa la saba na la nane wote watatumikia adhabu ya miaka
mitatu jela," alieleza Hakimu Mgeta
No comments:
Post a Comment