USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA NCHI HII YA TANZANIA
Rasilimali
ni vyanzo vya nchi ambavyo vinasaidia nchi kiuchumi ni zawadi
tuliyopewa na Mungu kama urith wa dunia.Nchi hii ya Tanzania tunazo rasilimali
nyingi ambazo ni; maadini, mbuga za wanyama, milima ,mito, maziwa, bahari na
vinginevyo vingi.Lakini tumeona rasilimali nyingi za nchi hii zikitumiwa na
wajanja wachache ambao hawalitakii mema taifa hili tungeona kama zingetumiwa
vizuri nchi ingefaidika na uchumi ungekuwa.
Sekta ya
madini: Madini ni rasilimali nzuri sana kama itatumiwa vizuri itanufaisha
watanzania kwani Tanzania tunayo madini ya aina nyingi kama; dhahabu alimasi,
makaa ya mawe na tanzanite ambayo inapatikana Tanzania pekee duniani.Tumeona
serikali imeshindwa kusimamia vizuri sekta hii ambayao itasaidia nchi kupiga
hatua,Naishauri serikali kuchunguza sekta hii kwani imejaa rushwa ufisadi
mkubwa ambao unasababisha nchi kuwa masikini kwa ajili ya watu wachache ambao
hawaitakii Tanzania mema.Madini ndiyo rasilimali ndiyo tuliyopewa na Mungu kama zawadi ya kututoa
kwenye shida.
Mbuga za
Wanyama; Tumeona mbuga mbuga zetu za wanyama kama
Ngorongoro, Manyara,Serengeti Mikumi pamoja na nyingine ambazo ni ndogo zipo
ndani ya nchi hii ni rasilimali ambazo huingizia serikali mapato mengi kwa utalii
na kusaidia uchumi kukua. Lakini tumeona sekta hii imekuwa na ubadhilifu mkubwa
wa Ruswa na Ufiksadi na kuiacha nchi ikiwa masikini.Wanyama wanatorooshwa na
kuuzwa nje pamoja na uwindaji holela ambao unafanywa na baadhi ya wananchi kwa
kushirikiana na viongozi ambao wanahusika na sekta hii.Naiomba serikali yangu
ichunguze hawa watu wachache wanaohujumu uchumi wa nchi kwa kuiibia serikali
katika rasilimali hii ya utalii ambayo inaingizia serikali fedha nyingi ambazo
zinasaidia uchumi kukua.
Milima yetu;
Milima ni mojawapo ya railimali ambazo hutuingizia fedha za kigeni kwa Utalii ambazo zinasaidia Taifa kusonga
mbele kwa kuua uchumi.Fedha hizi kama zinatumika vizuri zitasaidia kukuza
uchumi wa Taifa la Tanzania. Kuondokana na
umasikini,mlima Kilimanjaro meru na uluguru ni rasilimali za kujivunia kwa husaidia nchi ambayo ni
changa kama Tanzania kujikwamua kwenye dibwi hili la umaskini naomba serikali hii isaidie kusimamia fedha
hizi zinazopatikana kutokana na rasilimali hizi ambazo ni za wale tulopewa
mungu kama uridhi wan chi yetu ya Tanzania
Bahari yetu ya hindi hii ni moja wpo ya rasilimali
tuliyopewa na mungu kama zawadi kutoka kwa mungu lakini haitumiwi vizuri na
watanzania kwa kuchafua bahari na kutumia mabomu kuangamiza viumbe waliopo
ndani ya maji kama samaki dagaa pamoja na aina zote za wanyama waliopo ndani ya
bahari naiomba serikali isimamie vizuri Bahari yetu ya hindi na kukomesha
wavuvi haramu ambao halitakii taifa mema . Nchi inaweza uza samaki na dagaa na
kusaidia kukuza uchumi wa Taifa hili Pia Bahari yetu ni Moja wapo ya Utalii wa
kujitangaza kimataifa
Maziwa yetu: Maziwa yetu ndani ya nchi hii ni muhimiu sana kama rasilimali ya nchi tumeona kuna ziwa kama Victoria ambalo
maporomoko yake husaidia katika swala la umeme Pamoja na kutupatia samaki .
Gesi: Hii ni moja wapo ya rasili mali ya Taifa hili ambayo
inasaidia nchi kukua kiuchumi na kuwasaidia watanzania kupata Nishati ambayo
itawasaidia katika maswala yao ya kila siku Naishauri serikali kusimamia vizuri
rasilimali hii ya gesi ambayo inaingizia Taifa Hela Nyingi na kuinua Pato la
Taifa kukua na Kuondolea watanzania Umaskini uliotanda ndani ya macho ya
watanzania Serikali isikubali watu wachache watumie rasilimali hii muhimu
kujinufaisha wenyewe kwa kutumia nishati kama rasilimali ya wachache .
Makaa ya mawe: Nishati hii ni muhimu kwa kulisaidia Taifa
kiuchumi kwa kuongeza pato la Taifa naishauri serikali kusimamia nishati hii
muhimu na kuanza kuchimba ili iweze kuwanufaisha watanzania kama itakuwa
haiwanufaishi watanzania Haina haja ya kuchimbwa kwani itakuwa imewanufaisha
wachache Nishati hii ni muhimu kwani nchi inabaki maskini huku ikiwepo
Rasilimali Muhimu kama hii.
Sehemu ya Kitalii Zanzibar na Bagamoyo : Hii nimoja wapo ya
rasilimali inayotupatia fedha za kigeni kwa kuangalia mambo ya kale
yaliyofanywa na babu zetu. Na kutuachia ukumbusho wa vitu ambavyo ni vya
kukumbukwa na kuenziwa kama fahari ya nchi na
rasilimali ya kujivunia . Naishauri serikali kuwa makini kwa sekta hii imejaa
rushwa na kulikosesha Taifa fedha za Kigeni watalii wanaingiza fedha nyingi
Lakini hazionekani kwani zinaishia kwa wajanja wachache Kama
sekta hii itazibitiwa vizuri basi Taifa Litakuwa linanufaika na Rasilimali hii
muhimu tuliachiwa na Babu zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Mapango ya mboni Tanga:
Hii nayo ni moja wapo ya rasilimali ya nchi kwani nayo hutupatia fedha
za kigeni kama sehemu ya kitalii kwa maajabu ya mapango ya mboni Tanga tunaona
serikali inapata fedha nyingi kwa kivutio hiki ambacho husaidia kukuza uchumi
wa Taifa letu lakini kama hakutakuwa na usimamizi mzuri wa fedha inayopatika
wananchi watakuwa hawanufaiki na rasilimali hii ambacho ni kivutio cha wageni
na watu wa ndani kama sehemu ya uchumi wan chi.
Bonde la oldivai George: Hii ni moja wapo ya uridhi
tulioupata kwa babu zetu kama Historia ya nchi Tunajua Oldivai George ni bonde lililopatikana fuvu la binadamu wa
kwanza kuishi liligunduliwa huko arusha mwaka 1958 na Kuwekwa kwenye historia
ya nchi kama sehemu ya kitalii . Taifa limekuwa likipata fedha kwa kivutio hiki
ambacho kimekuwa kikisaidia kuinua uchumi wan chi. Naomba serikali yangu iwe
inasimamia vizuri mapato yanayopatikana kwani kufanya hivyo itawanufaisha umma
kunufaika na rasilimali za nchi hii.
Nimeona nizungumzie kuhusu usimamizi wa rasilimali za nchi
hii ya Tanzania
. Kwani ndio moyo wa wananchi na si rasilimali za viongozi wa umma peke yake
nchi hii kumekuwa na tabia moja ya rasilimali kufaidika na viongozi na kuacha
watanzania wakiishi maisha ya kimaskini huku migodi ikibaki mashimo tu. Na
kinachopataikana hakijulikani kinaenda wapi tumeona wanyama wetu wakiuzwa
kinyemela kwa ujanja wa wachache huku watanzania wakikosa rasilimali za nchi yao . Namuomba Mh. Jakaya
Mrisho Kikwete Kufuatilia swala hili la usimamizi wa rasilimali za watanzania
na kuhakikisha zinawanufaisha wananchi na si vigogo wachache wenye kukosa utu
na uruma kwa watanzania namsihi atoe adhabu kali kwa wale wanaopatikana na
makosa ya kuhujumu rasilimali za nchi hii na kuwafikisha kwenye vyombo vya
sheria akijaribu kuchukua hatua basi Taifa litasonga mbele na uchumi wa Taifa
hili utakuwa na Kustawi kwani wanaotusababishia umaskini ndani ya Taifa hili ni
wajanja wachache ambao wamekuwa sumu ndani ya nchi hii kwa kujinufaisha na
rasilimali za watanzania.
Mwisho nawasihi watanzania Wakati umefika wakujua kilicho
chao na kuambia Mafisadi, wala rushwa basi imetosha tumechoshwa na kutunyonya
kwa kutumia rasilimali zetu kwa maslahi yao
binafsi.
Ni mimi Mpenda Maendeleo:
DENIS BAHATI HENRY
Mungu ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Afrika.
0712 550508
0765 002472
TUNDU LISSU DHAMANA YAMTOA JELA
Kiongozi huyu asema jela panatisha,aomba haki za binadamu zifuatwe....
Mbunge wa Singida Mashariki kupitia CHADEMA, Tundu Lissu na wenzie saba
wameachiwa kwa dhamana ya sh. milioni 70 na kuambiwa wasifike eneo la
Nyamongo, Tarime ambapo yalitokea mauaji ya watu kadhaa.
Watu hao wameshitakiwa kwa makosa matatu yakiwamo ya kuvamia Hospitali
ya Wilaya ya Tarime kulimokuwa kumehifadhiwa maiti, na kufanya kusanyiko
pasipo halali.
No comments:
Post a Comment