OBAMA AMETAKA MAZUNGUMZO NA TALEBANI
Alipohojiwa na BBC, kabla ya kuanza ziara yake Uingereza Jumatatu, Rais
Obama ameonesha kuwa atakuwa tayari kuamrisha operesheni nchini
Pakistan, dhidi ya kiongozi mwengine wa Al Qaeda au Taliban.
Ingawa Rais Obama alisema yuko tayari kuchukua hatua dhidi ya Mullar
Omar kiongozi wa Taliban, lakini kauli yake ilikuwa tafauti kuhusu vita
dhidi ya Taliban nchini Afghanistan.
Alifahamisha wazi kuwa vita virefu kabisa vya Marekani vinaweza
kumalizika kwa mazungumzo na adui:
"Hatuwezi kumaliza tatizo hili kwa vita.
Tunachoweza kufanya ni kutumia mafanikio tuliyopata kijeshi kutafuta
suluhisho la kisiasa.
Inamaanisha kuwa hatimaye lazima tuzungumze na Taliban, ingawa tumeweka
shuruti kabla ya mazungumzo ya maana kufanyika.
Taliban lazima ikate uhusiano na Al Qaeda, iache kutumia nguvu, na
itabidi iheshimu katiba ya Afghanistan."
Reviewed by
crispaseve
on
2:41 PM
Rating:
5
No comments:
Post a Comment