Mh. Benjamin Mkapa,
apokea tuzo ya heshima.
Rais
mstaafu wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa,
akipokea tuzo yake ya heshima kutoka kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dk. Mohamed Gharib Bilal,
chama cha waandishi wa
habari za michezo (TASWA) kimempa mzee Kkapa tuzo hiyo maalum ya
heshima, kutokana na mchango wake katika michezo hasa ujenzi wa uwanja
mpya wa Taifa,
Mh Mkapa amesisitiza uwanja huo uendelee kutunzwa vyema
ili nchi yetu iendelee kuwa na kumbukumbu na urithi kwa vizazi
vijavyo,pichani kulia ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya
Serengeti (SBL) Teddy Mapunda.
Katika utoajiwa tuzo hizo mchezaji wa
jumla ni Mwanaidi Hassan anayecheza mchezo wa Netball katika timu ya
JKT Mbweni.
No comments:
Post a Comment