Hussein Mubaraka na watoto wake wawili kufikishwa mahakamani.
Kairo,
Misri 01/06/2011. Serikali ya Misri imetangaza ya kuwa aliyekuwa rais
wa zamani wa nchi hiyo atafikishwa mahakamani yeye na watoto wake kujibu
mashitaka ya kusababisha maafa yaliyo tokea wakati wa maandamano ya
kutaka ang'olewe madarakani kwa rais huyo.
Kwa
mujibu wa habari kutoka serikali zinasema " Hussein Mubaraka na watoto
wake wawili wa kiume watafikishwa mahakamani kuanzia tarehe 13, mwezi wa
nane."
Habari hizo pia
zilisisitiza yakuwa ikiwa "Hussein Mubaraka atakutwa na hatia ya
kuhusika na machafuko yaliyo sababisha mauaji wakati wa kutaka atolewe
madarakani baada ya kutawala Misri kwa muda wa miaka 30, basi huenda
akaukumiwa adhabu ya kifo."
Rais Hussein Mubaraka alitolewa madarakani baada ya maandamano yaliyo chukua siku 18 ya kutaka atoke madarakani.
Mshukiwa wa mauaji ya Serbia,Meja Ratko Mladik kupelekwa Uhollanzi.
Mshukiwa wa mauaji ya Serbia, meja Ratko Mladik kupelekwa Uhollanzi.
Belgrade,
Serbia - 31/05/2011.Mahakama kuu nchini Serbia imekataaa na kuitupilia
mbali rufaa ya mshukiwa na muhusika mkuu wa mauaji ya liyo tokea
wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyo tokea miaka ya 1991-95.
Mtuhumiwa
huyo Ratko Mladik, ambaye alikuwa mkuu wa majeshi anakabiliwa na
mashitaka ya dhidi yake kwa kuhusika na mauaji ambayo yalisababishwa na
vita hivyo, wakati yeye akiwa kama mkuu wa majeshi.
Kufuatia
kukataliwa rufaa hiyo, mkuu wa majeshi huyo Ratko Mladik, anatarajiwa
kupelekwa kwenye mahakama kuu ya kutetea haki za binandamu iliyopo
nchini Hollanzi ili kujibu mashitaka yanayo mkabili.
Hata
hivyo kabla ya kupelekwa nchini Uhollanzi, Ratko Mladik, aliruhusiwa
kutembela kaburi la mwanaye wa kike ambaye alijiua baada ya baba yake
kushutumiwa ya kuwa anamehusika katika mauaji.
Rais wa Soka asema hakuna shaka ni matatizo ya muda.

Zurich,
Switzaland - 30/05/2011 Rais wa shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu
duniani FIFA, amekataa ya kuwa shirikisho hilo lipo na mvutano ndani ya
uongozi wake.
Sepp
Blatter, alisema "shirikisho hilo halina mvutano na matatizo yalito
tokea ni kutokana na mlolongo wa shutuma ya kuwa ndani ya shirikisho
hilo kuana milungura na rushwa ambazo zimefanyika na matatizo yaho ni ya
muda yatatafutiwa uvunbuzi."
Rais
huyo wa FIFA anatarajiwa kuwa mgombea pekee wa kiti cha urais baada ya
mpinzani wake Mohamed bin Hammam kujitoa kutokana na shutuma hizo za
rushwa.
Rais wa Afrika ya Kusini kutafuta suruhisho kati ya Walibya.
Kwa
mujibu wa habari kutoka ofoce ya rais zinasema, "rais Jokob Zuma
atakuwa nchini Libya ili kuongea na kujadiliana na kiongozi wa Libya
Muammar Gaddafi ili kusimamisha mapigano.
hata
hivyo kundi la upinzani lenye makao yake makuu Benghazi limesma"
inaelekea kuwasili kwa rais wa Afrika ya Kusini kunaleta utata, kwani
mpaka sasa hakuna dalili za au amelezo ya kuwa Muammar Gaddafi atatoka
madarakani na kuondoka.".
Kuwasili
kwa rais wa Afriaka ya Kusini nchi Libya kunatazamiwa kuleta maono
tofauti ambayo huenda ya leta mabadiliko katika kampeni nzima ya
kidemokrasi nchini Libya
Hatimaye Ratko Mladic akamatwa.
Belgradi, Serbia- 26/05/2011. Serikali ya Serbia imetangaza kukumatwa kwa aliyekuwa mkuu wa jeshi Bosnia Serbi ambaye anakabiliwa na mashitaka ya mauaji wakati wa vita vilivyo tokea mwaka 1992-95. Generali Ratko Mladic ambaye alikuwa natafutwa ili ajibu amshitaka dhidi yake, alipotea mara baada ya kesi dhidi yake kufunguliwa na mahakama ya kimataifa. Akitangaza kuhusu kukumatwa huko, rais wa Serbia Boris Tadic alisema "kwaniaba ya wanchi wa Serbia napenda kuwatangazia ya kuwa Ratko Mladic amekamatwa, na kuanzia sasa tunafungua kitabu kipya ambacho kitatuwezesha kusamehena na kukubaliana kuishi pamoja." "Na tunahaidi wale wote wafanyao mabaya lazima watajibu mashitaka"alimalizia kwa kusema haya rais wa Serbia Kwa mujibu wa habari zilizo patikana zinasema "Ratko Mladic hakuwa na matata au kuleta kipingamizi wakati wakukamatwa kwake na inasemekana anamatatizo katika moja ya mkono wake."
Serikali ya Libya kuitaka Uhispania katafuta njia ya luleta amani.
Madrid, Uhispania -
26/05/2011.Serikali ya Uhispania imepokea maombi kutoka serikali ya
Libya ya kutaka kuwepo na mazungumzo ya kusimamisha vita vinavyo endelea
nchini Libya.
Habari kutoka ofosi ya waziri mkuu wa Uhispania, zinasema " tumepokea
mswaada kutoka serikali ya Libya ambao unaomba kuwa na mazungumzo ya
kuleta amani nchini Libya."
Akiongea mbele ya waandishi wa habari, waziri mkuu wa Libya Al-Baghdadi
al Mahmoud "alisema serikali ya ke ingependelea kuanza mazungumzo ya
kuleta amani na kusimamisha mashambulizi nchini Libya yanayofanywa na
NATO."
"Na Muammar Gaddafi bado na atakuwa kiongozi wa LIbya, na kama Gaddafi
akiondolewa kwa kutumia nguvu, basi hakutakuwepo na Libya watu wanayo
tarajia."
Hata hivyo, kundi la upinzani linalo pinga serikali ya Gaddafi, linadai
lazima kiongozi huo ataoke madarakani na ndipo amani ipataikane.
This Blog is all about Social and Entertainment issues... Karibu kwenye sehemu yetu ya kujidai!!!
No comments:
Post a Comment