Header Ads

NDOA YA ARNOLD SCHWAZNIGGER KUVUNJIKA.

  

Sababu ni mtoto wa nje aliyezaa na mfanyakazi wa nyumbani kwake miaka 10 iliyopita.Mwanamke anaitwa Mildread Baena walifanya mapenzi na Shwaznigger nyumbani kwenye nyumba anayoishi na familia yake.Hata wakati wa ujauzito bibie aliendelea kufanya kazi katika nyumba hiyo.

Kweli moyo wa mtu ni kichaka,jamaa alikaa kimya miaka yote hiyo mpaka hii majuzi alipomueleza mkewe.Wadadisi wa mambo wanasema ndio sababu zilizopelekea ndoa yake ya miaka 25 na mkewe Maria Shriver kuvunjika.Tarehe 9 mwezi huu wanandoa hao walitangaza kutengana na tarehe 17 Shwaznigger akaomba msamaha kwa kuwa na mtoto na mwanamke huyo aliyekuwa mfanyakazi nyumbani kwao.

No comments:

Powered by Blogger.