Mke
wa rais aliyeondolewa madarakani wa Misri Hosni Mubarak, aliyekuwa
akishikiliwa kwa makosa ya ulaji rushwa, ameachiwa kwa dhamana baada ya
kukabidhi mali zake.
Maafisa
walisema Suzanne Mubarak alikabidhi nyumba ya kifahari iliyopo kwenye
kitongoji cha mjini Cairo na fedha zenye thamani ya dola za kimarekani
milioni 3 zilizoshikiliwa kwenye akaunti mbalimbali za benki nchini
Misri.
Familia ya Bw Mubarak inakabiliwa na madai ya "kupata mali kinyume cha sheria" wakati alipokuwa madarakani kwa miaka 30.
Bw Mubarak aliyeondoshwa
madarakani mwezi Februari pia anashutumiwa kuhusika katika mauaji ya
waandamanaji waliopinga uongozi wake.
Watoto wake wawili wa kiume, Alaa na Gamal, kwa sasa wanashikiliwa kwenye gereza la Tora kwa makosa ya udanganyifu.BBC |
No comments:
Post a Comment