UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116539
E-mail: press@ikulu.go.tz
Website: www.mawasilianoikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 | PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mmoja wa Wizara, na Naibu Makatibu Wakuu
10 wa Wizara mbalimbali.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha Naibu Katibu Mkuu mmoja kutoka Wizara moja kwenda nyingine.
Taarifa
iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Aprili 27, 2011, na
Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi Bwana George Yambesi inasema kuwa uteuzi huo
wa maofisa hao waandamizi wa Serikali unaanzia Alhamisi iliyopita,
Aprili 21, mwaka huu, 2011, na wataapishwa Jumamosi wiki hii, Aprili 30,
saa sita mchana.
Taarifa
hiyo inasema kuwa katika uteuzi huo, Rais Kikwete amemteua aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Bwana Job
D. Masima kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Aidha,
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amemhamisha Injinia
Mbogo Futakamba aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji kwenda Wizara
ya Kilimo, Chakula na Ushirika.
Taarifa hiyo inasema kuwa Naibu Makatibu Wakuu walioteuliwa na Mheshimiwa Rais ni kama ifuatavyo:
· Bwana
Aphayo Kidata ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ikulu. Kabla ya uteuzi
wake, Bwana Kidata alikuwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango katika Wizara
ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
· Bwana
Hab Mkwizu ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Menejimenti ya Utumishi wa
Umma. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mkwizu alikuwa Karani wa Baraza la
Mawaziri.
· Bwana
Charles Amos Pallangyo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya
Waziri Mkuu. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Pallangyo alikuwa Mkurugenzi wa
Uratibu – Ofisi ya Waziri Mkuu.
· Bibi
Mwamini Juma Malemi ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi. Kabla ya hapo alikuwa Msaidizi wa Makamu wa Rais
katika masuala ya Maendeleo ya Jamii na Uratibu wa Malalamiko ya Jamii
na Uratibu wa Malalamiko ya Wananchi.
· Injinia
Mussa Ibrahim Iyombe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Ulinzi na JKT. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Miundombinu ya
Usafiri katika Wizara ya Ujenzi.
· Injinia
Dkt. John Stanslaus Ndunguru ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika
Wizara ya Ujenzi. Kabla ya hapo, alikuwa Mkurugenzi wa Huduma na Ufundi
katika wizara hiyo hiyo ya Ujenzi.
· Bwana
John Thomas James Mngodo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika
Wizara ya Uchukuzi. Kabla ya uteuzi wake alikuwa Mkurugenzi wa Usalama
wa Chakula.
· Bibi
Anna T. Maembe ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Kabla ya uteuzi wake, Bibi Maembe
alikuwa Mkurugenzi wa Mazingira na Habari wa NEMC.
· Bibi
Sihaba Nkinga ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo. Kabla ya hapo alikuwa Mkurugenzi
wa Sera na Mipango katika Wizara ya Uchukuzi.
· Injinia
Bashir J. Mrindoko ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya
Maji. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Mrindoko alikuwa Kamishna wa Nishati
na Mafuta ya Petroli.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
27 Aprili, 2011
No comments:
Post a Comment