Header Ads

YANGA BINGWA 2010/2011




BAO la kisigino la kiungo wa Yanga, Nurdin Bakari lilitosha kufuta ndoto ya Simba ya kutetea ubingwa wake pamoja karamu ya mabao ya 4-1  waliyoipata dhidi ya Majimaji ya Songea.

Nurdin akionyesha nia halisi ya kuifanya Yanga bingwa, huku akiwa amelipa mgogo goli alipopokea mpira uliokuwa ukizagaa kwenye eneo la hatari la Toto Africans ya mjini Mwanza, na kupiga kisigino huku akimwacha golikipa wa Toto Afrika, Hussein Tade aliyeingia kuchukua nafasi ya Wilbert Mwate akiruka upande wa kulia na mpira ukipita alipotoka kuipa Yanga bao la tatu. Bao hilo ni zuri na uenda likawa bao zuri la msimu ambao Yanga kweli wamepigana kiume kurudisha ubingwa huu nyumbani.

Kipa Tade aliingia uwanjani dakika ya 83 kuchukua nafasi ya Mweta aliyekuwa kikwazo kikubwa kwa Yanga, baada ya kuumia paja.

Mabingwa hao wapya walianza mchezo huo taratibu na kuifanya Toto kutawala sehemu kubwa ya kipindi cha kwanza, lakini mambo yalibadilika nusu ya pili na kufanikiwa kupata mabao matatu muhimu.

Kabla ya kiungo Bakari kuipatia Yanga bao la kuongoza dakika ya 46, kwa mpira wa adhabu nje ya eneo la 18, uliogonga ukuta na kutinga wavuni.

Naye mshambuliaji Davies Mwape alifunga bao lake 8 msimu huu la pili kwa Yanga dakika 63, akiunganisha krosi ya Shadrack Nsajigwa, katika harakati za kumzuia nahodha huyo wa Taifa Stars, beki wa Toto Laban Kambole aliumia na kutolewa nje.

Awali mshambuliaji Mwape nusura aifungie Yanga bao la mapema dakika ya tisa baada ya shuti lake kugonga mwamba na kutoka nje.

Kipa wa Yanga, Yaw Berko alipewa kadi ya........ kwa habari zaidi..bonyeza hapa 

No comments:

Powered by Blogger.