Header Ads

BONGO STAR SEARCH 2010

Shindano la kumtafuta Bongo Star(mpya) katika muziki linaendelea. Shindano hilo lilianza tarehe 17 Julai na linaendelea mpaka tarehe 12 Agosti.Vipindi vya televisheni vitaanza kuonyeshwa kupitia Kituo cha Televisheni cha ITV kila Jumapili kuanzia tarehe 28 August mpaka mwisho wa shindano hilo.
Pichani ni majaji wa shindano hilo.Kutoka kushoto ni Espen Sorensen au maarufu kama Mzungu Kichaa. Yeye alizaliwa nchini  Denmark na kisha akakulia Tanzania baada ya kuhamia hapa akiwa na miaka 6 kutokana na wazazi wake kuhamishiwa Tanzania kikazi.Ameshiriki katika harakati za muziki wa Hip Hop nchini Tanzania kwa muda mrefu.Hivi karibuni kwa kushirikiana na Proffessor Jay,alifyatua kibao Jitolee ambacho kilimweka katika chat za muziki kwa namna nyingine kabisa.
Katikati ni Rita Paulsen au Madame Rita kama anavyofahimika kwa wengi. Yeye ni Mkurugenzi wa Benchmark Productions ambao ndio waanzilishi wa shindano hilo.BC iliwahi kufanya naye mahojiano.Unaweza kuyasoma hapa.
Kulia mwa picha ni Joachim Kimaryo au maarufu kama Master Jay.Huyu ni Producer wa muda mrefu sana nchini Tanzania.Mwaka 1996 alianzisha studio ya MJ Records ambayo imekuwa chimbuko la wasanii wengi nchini Tanzania.
Kwa habari zaidi juu ya shindano hili: Bongo Star Search.

No comments:

Powered by Blogger.