UCHIMBAJI WA MCHANGA KWENYE MITO DAR ES SALAAM WAPIGWA MARUFUKU.
Waziri
wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(OR-TAMISEMI), Mhe Selemani Jafo (Mb) amepiga marufuku uchimbaji wa
mchanga unaoendelea katika mito mbalimbali Jijini Dar es Salaam.
Mhe.
Jafo ametoa katazo hilo wakati wa ziara yake ya kuangalia athari
zilizotokana na mafuriko katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilala leo 20
Aprili 2018. Akiwa
katika kata ya Gongolamboto eneo la Ulongoni A na Ulongoni B, amejionea
jinsi ambavyo mafuriko yaliyotokana na wingi wa mvua zilizonyesha
yalivyoharibu madaraja na kuacha athari kubwa kwa wananchi.
“Nimejionea
mwenyewe jinsi ambavyo mvua hizi zimeleta athari kubwa hapa na
kusababisha mawasiliano kukatika baina yenu nyinyi na wenzenu wa upande
wa pili. Lakini niwaambie kuwa kwa sehemu kubwa baadhi ya wananchi
wanachangia uharibifu wa maeneo haya kutokana na uchimbaji wa mchanga
unaoendelea na kusababisha uharibufu katika kingo za mito pamoja na
miundombinu hii iliyojengwa,” alieleza Mhe. Jafo
Waziri
ameeleza kuwa miundombinu inajengwa kwa gharama kubwa na Serikali
lakini wapo watu ambao wanaiharibu kwa makusudi kutokana na uchimbaji wa
mchanga, hivyo akaeleza kuwa Serikali haitavumilia swala hilo.“Hatuwezi
kuzizuia mvua zisinyeshe lakini hatuwezi kuvumilia kuwaacha watu
wanaoharibu miundombinu na kingo za mto kwa kuchimba mchanga. Hivyo
kuanzia leo napiga marufuku uchimbaji wa mchanga katika maeneo yote ya
mito ya Dar es Salaam,” ameagiza Waziri Jafo.
Amemuagiza
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe. Sofia Mjema aliyeambatana naye katika
ziara hiyo kusimamia agizo hilo pamoja Mkoa wa Dar es Salaam kwa ujumla
wake, na kuwakamata wale wote watakaokaidi agizo hilo.Aidha
Mhe. Jafo ameeleza kuwa Serikali inajitahidi kurejesha mawasiliano
katika maeneo hayo yaliyoathirika kwa kujenga madaraja ya muda wakati
wakisubiri ukarabati mkubwa kufanyika.
Ameeleza
kuwa amewasiliana na waziri wa Ulinzi Mhe. Hussein Mwinyi ili Jeshi la
Ulinzi lisaidie katika kutengeneza madaraja hayo. “Waziri
wa Ulinzi ameniahidi kuwa anatuma wataalamu wa Jeshi kufanya tathmini
ya uharifu ili kutengeneza madaraja hayo ya muda,” amesema Jafo.Awali,
katika ziara hiyo Mhe. Jafo ametembelea Mradi wa Mabasi Yaendayo Kasi
“DART” katika kituo cha Jangwani na kuangalia athari zilizoltokana na
mafuriko.
Akiwa
katika kituo hicho cha Jangwani amepongeza uongozi wa UDART kwa
kuzingatia agizo lake alilolitoa awali la kuyahamisha mabasi katika
kituo hicho na kuyalaza Kimara pamoja na Gerezani hivyo kufanikiwa
kuokoa mabasi hayo.“Mmeniambia
kuwa yale mabasi niliyoyaona hapa wakati wa mafuriko ni yale ambayo
yalikuwa hayatembei kabisa na hata hivyo mmetoa vifaa amabavyo
vingeharibika katika mabasi hayo na mengine yote mliyatoa hapa.
Nawapongeza kwa hilo,” ameeleza Jafo.
Mhe.Jafo
amesema kuwa mafuriko hutoke duniani kote marekani, china na kwingineko
na hatuwezi kuyazuia, lakini ni akasema kuwa ni lazima wadau na
wananchi wote wazingatie tahadhari zinazotolewa ikiwa ni pamoja na
kuhama mabondeni ili kupunguza athari.Pia
ameeleza kuwa Serikali inampango mkubwa wa kuutengeneza Mto Msimbazi
kupitia Mradi wa DMDP, ambapo takribani dola za kimarekani 20 milioni
zimetengwa ili kupata suluhisho la kudumu. Alieleza kuwa kazi hiyo
inatarajiwa kuanza mwezi Septemba, 2018 mara baada ya kumalizika kwa
usanifu.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
Selemani Jafo akiwa na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa wilaya ya Ilala
Sophia Mjema wakionyeshana maeneo ya daraja yalivyo haribika na
mafuriko.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi)
Selemani Jafo akiwa na viongozi wengine katika ukaguzi wa athari za
mvua.
Maeneo yaliyoharibiwa na Mvua
Maeneo yaliyoharibiwa na mvua
Maeneo yaliyoharibiwa na mvua
Maeneo yaliyoharibiwa na mvua
Athari za mafuriko
No comments:
Post a Comment