OBC yatoa magari 15 kwa wizara ya maliasili
Magari 15 yaliyokabidhiwa na Kampuni ya OBC ya Loliondo.
Mkurugenzi
idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina akikata utepe kuashiria uzinduzi wa
magari 15 aina ya Toyota Land cruiser yenye thamani ya shilingi Billion
1.5 yaliyotolewa na kampuni ya uwindaji ya OBC,ya Loliondo kwa ajili ya
shughuli za kuzuia ujangili na uhifadhi. Hafla hiyo ilifanyika jana jiji
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina akijaribu kuendesha moja ya magari 15
aina ya Toyota Land cruiser yenye thamani ya shilingi Billion 1.5
yaliyokabidhiwa na kampuni ya uwindaji OBC,ya Loliondo kwa ajili ya
shughuli za kuzuia ujangili na uhifadhi. Hafla hiyo ilifanyika jana jiji
Dar es Salaam
KAMPUNI
ya uwindaji ya Otterlo Business Corporation Limited (OBC) imekabidhi
magari 15 kwa wizara ya maliasili na Utalii kwa ajili ya kusaidia
kulinda rasilimali ya wanyamapori nchini.
Magari
hayo aina ya Toyota Landcruiser yalikabidhiwa jana kwa Mkurugenzi wa
idara ya wanyamapori, Nebbo Mwina,katika ofisi za Wizara ya Maliasili,
jijini Dar es Salaam.
Akikabidhi
magari hayo yenye thamani ya Zaidi ya sh. Bilioni 1.5, Mkurugenzi
msaidizi wa OBC, Molloimet Yohana, alisema kuwa msaada huo ni mahususi
kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye mapambano dhidi ya ujangili na ulinzi
wa wanyamapori.
“Huu
ni mwendelezo wa azma ya serikali ya UAE na OBC katika kuunga mkono
mapambano hayo kwani tumekuwa tukifanya hivyo mara kwa mara,”alisema.Alisema
ushiriki wao katika uhifadhi wanyamapori utaendelea kwani ni mpango
endelevu na kamwe hawatasita kusaidia pale itakapobidi.Akipokea
msaada huo, Mwina alisema serikali inatambua mchango mkubwa wa OBC
ambao imekuwa ikitoa katika sekta hiyo,na kuwataka kuendeleza mahusiano
na kutokatishwa tamaa na maneno yanayozungumzwa juu ya kampuni hiyo.
“Napenda
kusema kwamba OBC tumekuwa na mahusiano na nyinyi ya muda mrefu
tumepata misaada yenu kwa muda mrefu kwa hiyo mahusiano yenu na sisi ni
ya muda mrefu na ni mazuri hivyo tunawaomba kwamba muendeze hayo
mahusiano yenu msikate tamaa tunajua kuna maneno yanasemwahuku na kule
yakijaribu kuwakatisha tamaa juhudi zenu naomba msikate tamaa kwa hayo
maneno ambayo yanasemwa Chini chini “Alisema
Alisema
ni vyema OBC ikawapuuza watu ambao wamekuwa wakisema kampuni hiyo
hafanyi kazi yake inavyotakiwa lakini wao kama wizara tunatambua kwamba
wamekuwa ni msaada msaada mkubwa kwa serikali na uhifadhi.
Akishukuru
kwa msaada huo mkurugenzi wa mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini
(TAWA )Dk. James Wakibara alishukuru OBC kwa msaada huo ambao alisema
utarahisisha utendaji kazi wa mamlaka hiyo ambayo inakabiliwa na
changamoto ya rasilimali fedha,watu na vifaa.
“Lazima
tutoe shukrani zetu za dhati kwa uongozi wa OBC kwanza kwa kufikiria
hili wazo lakini pia kwa kujitoa,nguvu waliyoifanya,jitihada
walizozifanya,matumizi waliofanya hadi leo tunapata hivi vifaa ambavyo
vitatusaidia mtufikishie salam zetu kwa mkurugenzi ambae hakuweza kufika
lakini Mwambie tunashukuru na Tunaheshimu kwa msaada huu
uliotolewa.”alisema
Amesema
gari ni kitu mihimu sana katika shughuli ya uhifadhi kwa sababu
inawezesha kufika mahali popote kwa kuwa ni vigumu sana kulinda mapori
kwa kutembea kwa miguu.
“Ni
vizuri kwamba mtu anapokusaidia lazima atakuwa amewaza hapa kuna tatizo
kwa hiyo katika tatizo hili na mimi nisaidie,kwa hiyo ule moyo tu wa
kusema kwamba niwasaidie wenzangu Ndio hazina kubwa kuliko hata kile
kilichotolewa”,alisema Dk.Wakibara.
No comments:
Post a Comment