Header Ads

RAIS DKT MAGUFULI AZINDUA MRADI MKUBWA WA MAJI NGURUKA WILAYANI UVINZA MAPEMA LEO.

Rais Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia Wananchi mbalimbali wa mji wa Nguruka mapema leo asubuhi,waliojitokeza mapema leo kumshuhudia Rais akiweka jiwe la msingi la Mradi wa maji.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,ambapo pia ameweka jiwe la msingi la mradi huo unaotarajia kukamilika Desemba 31, 2017,ukamilishwaji wa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akipeana mkono na Mbunge wa jimbo la Kasulu Mjini,Mh Daniel Nsanzugwako mara baada ya kuweka jiwe la msingi la Mradi mkubwa wa maji mapema leo mjini Nguruka mkoni Kigoma.Rais Magufuli ametekeleza ahadi yake ya kuupatia maji mji wa Nguruka Wilayani Uvinza Mkoani Kigoma,na kuwamba Mradi huo unatarajia kukamilika Desemba 31,2017,kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.
 Rais Dkt Magufuli akitoka kukagua mradi huo wa maji unaotarajia kukamilika Desemba 31,2017.kukamilika kwa mradi huo utamaliza tatizo la maji la Mji wa Nguruka.Rais Dkt Magufuli yuko njiani akielekea mkoani Tabora,ambapo atasimama Wilayani Kaliua na kuzindua barabara ya Kaliua hadi Kazilambwa yenye urefu wa kilometa 56.

No comments:

Powered by Blogger.