MASHAMBA YA MPUNGA YA MBARALI NA KAPUNGA YAPEWA ONYO KALI NA KIKOSI KAZI CHA KITAIFA CHA MTO RUAHA.
Kampuni inayojishughukisha na kilimo cha Mpunga ijulikanayo
kwa jina la Highland Estates iliyopo wilayani Mbarali mkoani Mbeya
imepewa agizo na Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha
kilichoko mkoa wa Mbeya kuwa ndani ya mwezi mmoja wahakikikishe wamesafisha
mifereji yote inayozunguka ndani ya shamba lao kwa kujenga upya miundombinu inayopoteza maji
, kung'oa magugu maji na nyasi zote
zilizoota katika mifereji ya matoleo ya maji ndani ya shamba hilo kwani
inazuia maji kupita kwa urahisi kuelekea Mto ruaha kama inavyotakiwa. Pia
wametakiwa kuanza taratibu za kupatiwa cheti cha ukaguzi wa athari za mazingira
kitoka Baraza lau Usimamizi wa mazingira (NEMC).
Akiongea katika ziara hiyo Mwenyekiti wa kikosi kazi hiko Bwana Richard Muyungi alisema Uongozi wa
shamba hilo wafanye juhudi za ziada kutunza mazingira yote yanayozunguka shamba
hilo na kuhakikisha maji yanapita kwa urahisi katika mifereji ya matoleo ya
kupeleka maji mto Ruaha Mkuu. "Tunawapa mwezi mmoja mfanye ukarabati na mrekebishe hali ya usafi
katika mifereji ya shamba lenu baada ya muda huo tutarudi kwa ajili ya
kukagua." Alisema Muyungi
Kikosi kazi hiko pia kilitembelea katika shamba la Mwekezaji
lililopo wilaya ya Mbarali Mkoani Mbeya lijulikanalo kama Kapunga Rice Project.
Kikosi kiliona matumizi mabaya ya maji kwa kuyachepusha bila vibali kunakofanywa na Wananchi walio maeneo ya
jirani. Badala ya mifereji ya maji iliyopo
shambani hapo kurudisha maji mto Ruaha Mkuu.
Maeneo mengi ya mifereji ya kutolea maji katika shamba hilo na
kupeleka mtoni yamezibwa kwa viroba na udongo ili maji yasiende mto Ruaha. Kikosi
kazi kilielekeza Kamuni michepusho yote
ya maji ifungwe mara moja na Kampuni isimamie na kugharamia shughuli hiyo. Maagizo hayo yote yametakiwa kukamilika mpaka
siku ya jumanne ya tarehe 25 Aprili 2017.
Kikosi kazi hiko cha Kitaifa kilichopo Mkoani Mbeya bado
kipo katika ziara ya kutembelea sehemu mbalimbali ili kujua, kufahamu, kuona na
kupata maoni mbalimbali ya Wananchi ni nini haswa kinachosababisha maji
kutokuingia katika mto Ruaha ili kutoa suluhisho la kudumu.
Mfereji wa kutolea maji kupeleka mto Ruaha Mkuu ulioko ndani ya Shamba
la Mpunga la Kapunga ukiwa umejengewa tuta ili kutopitisha maji hayo
kuelkea mto Ruaha kama inavyotakiwa
Magugu na nyasi zikionekana katika mfereji wa kupitishia maji katika shamba la Mbarali ambapo magugu hayo huzuia maji kutopita kwa urahisi.
Mwenyekiti wa kikosi kazi cha Kitaiaf cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Bwana
Ricahrd Muyungi akitoa maelekezo na maagizo kwa Wamiliki wa mashamba ya
mpunga ya Highland Estates juu ya wanachotakiwa kufanya baada ya shamba
alo kukutwa chafu sana na mifereji yao yote imejaa magugu maji.
No comments:
Post a Comment