Header Ads

BALOZI WA KUWAIT , JASEM AL-NAJEM AZINDUA VISIMA VINNE KATIKA SHULE NNE ZA MSINGI MANISPAA YA ILALA


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii

Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam jana.

Shule za Msingi zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja , Mwale pamoja na Bwawani

Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndio maana wameona umuhimu wa visima hivyo katika shule hizo.

Amesema wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika jamii kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.

Al-Najem amesema kuwa wamefanikiwa kuchimba visima 16 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 63,000 na watu wengine wanaweza kujitokeza kusaidia jitihada mbalimbali .

Ubalozi huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani sh.milioni tatu.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji katika shule ya Yombo iliyopo Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam jana, Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem kushoto na Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi wakinywa maji mara baada kuzindua kisima katika shule ya msingi Yombo jana jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala , Hamisi Mlangala akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada huo jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni jana jijini Dar es Salaam. 
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Amana jana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akimsikiliza Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni jana jijini Dar es Salaam.

No comments:

Powered by Blogger.