Mbowe apingwa kila kona,Ni kuhusu kubeza juhudi za Serikali Kagera
*Wasomi wamshukia, wamtaka aache siasa
WADAU
mbalimbali wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwa muwazi kwa wananchi wake wakati
wanapohitaji misaada mbalimbali wakati wa majanga.
Wametoa
kauli hiyo leo jijini Dar es salaam wakati wa mahojiano na mwandishi wa
habari hizi kueleza kauli ya hivi karibuni ya Mwenyekiti wa Taifa wa
Chadema, Freeman Mbowe ambaye amekaririwa akidai kuwa kauli za Rais
mkoani Kagera ni za hatari.
Wamesema
kuwa baadhi ya Watanzania wamezoea kupewa ahadi ambazo kwa wakati
mwingine ni vigumu kutekelezeka na sasa watu kama Mbowe bado wako kwenye
mtazamo huo.
Wameongeza
kuwa Rais Magufuli amekuwa siku zote mkweli, jambo ambalo baadhi ya
watu wasiopenda ukweli wanapotosha kauli zake kwa kutaka kuwachonganisha
wananchi na Rais wao ambaye amekusudia kuwaletea wananchi maendeleo.
Rais
Magufuli akiwa Kagera hivi karibuni alisisitizia msimamo ambao si mpya,
umekuwa msimamo wake na wa Serikali tangu yalipotokea maafa ya tetemeko
la ardhi mkoani humo kwamba Serikali itasaidia lakini haitaweza
kumjengea nyumba kila mtu.“Baadhi ya wanasiasa na viongozi wamekuwa
wakitoa kauli zenye kupotosha na kubeza hotuba ya Rais Magufuli mkoani
Kagera jambo ambalo sio zuri na sio ukomavu wa kiasa” walisema.
Mhadhiri
Mwandamizi Chuo Kikuu cvha Dar es Salaam, Dkt Bashiru Ally amesema kuwa
katika mfumo wa siasa huru kuna kutofautiana mitazamo kati ya wananchi
,Serikali na viongozi wa siasa lakini ni wazi kuwa Rais alisimama katika
msimamo wa Serikali yake na uwezo wa kutekeleza ahadi zake.
Alisema
kuwa Rais Magufuli alikuwa na maana nzuri ya kukabiliana na majanga
nchini inategemea uwezo wa nchi na mshikamano wa wananchi na huo ni
ukweli ambao wengi hawakupenda kuusikia.
Dkt.
Bashiru Ally alisema kuwa kwa janga la Kagera kulikuwepo mshikamano wa
Serikali katika ngazi zote, wananchi na wadau mbalimbali walishiriki kwa
namna moja ama nyingine kukabiliana na janga hilo.
“Wito
wangu ni kuwataka wanasisa kujifunza kutokana na majanga badala ya kutoa
kauli tatanishi na zenye kubomoa mshikamano wa wananchi, bali
wanatakiwa kukosoa bila kubeza, kupotosha kwa namna ni ya kungwana,”
alisema Dkt Bashiru
Kwa
upande wake Dkt. Benson Bana kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam amesema
kuwa watu wanatafsiri vibaya maneno ya Mhe. Rais aliyoyaongea Mkoani
Kagera hivi juzi.
“Mheshimiwa ameongea ukweli kwa sababu ni sahihi kuwasaidia watu wengi kwa pamoja kuliko kumsaidia mtu mmoja mmoja,” alisema.
Aliongeza
kuwa hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya lugha za Mhe. Rais kwani
lugha zake hazina ubabaishaji ni za kweli na ziko moja kwa moja, hao
wanaomuongelea vibaya ni wale wenye lengo la upinzani tu na sio
maendeleo ya Taifa.
Ameongeza
kuwa kwa upande wake pamoja na wananchi wenye mapenzi ya kweli
wamemuelewa Mhe. Rais na ndio maana walikuwa wakimpigia makofi wakati
akiongea kule Kagera.
”Mimi
nilikuwepo mkoani Kagera na hotuba za mheshimiwa zote nilizisikiliza kwa
makini ndio maana nasema wanye nia mbaya na Rais ndio wanaoongea mabaya
juu yake kwani mbona alivyoongelea suala la kupunguza umeme hawakusema
chochote?” alihoji Dkt. Bana.
Kwa
upande wa Mwenyekiti wa Chama cha United Democratic Party (UDP) John
cheyo amewataka Watanzania kutotegemea serikali kwa kila kitu pindi
wanapopatwa na majanga.
Alisema
kuwa lengo la Mheshimiwa Rais Magufuli ni kutaka Watanzania kujenga
utamaduni wa kujitegemea pindi wanapofikwa na majanga mbalimbali na ndio
maana alitaka kujua juhudi zao kabla ya kuomba msaada wa Serikali.
Profesa
Haji Semboja alisema kuwa kauli ya Rais ilikuwa ni kuwahimiza watu wa
Kagera ambao anajua wana uwezo wa mambo mengi ya kulima mazao mbalimbali
kama vile mazao ya chakula na biashara ikiwemo ndizi na kahawa ambayo
yanaweza kuwapatia chakula cha kutosha wananchi wa mkoa huo.
Naye
Kaimu Mkuu wa Chuo cha Diplomasia nchini Dkt. Bernad Achiula amesema
kuwa baadhi ya wananchi wamepokea hotuba ya Rais John Magufuli kwa
mtazamo tofauti, lakini ni dhahiri hakuna nchi yeyote duniani ambayo
inahudumia kila mwananchi katika majanga ya kiasili yanayotokea.
“Wajibu
wa Serikali katika nchi yeyote ni kujenga na kuboresha miundombinu
mbalimbali iliyotokea ikiwemo barabara, hospitali, shule, malazi ya muda
kwa waadhirika, madawa, miundombinu ya umeme, maji kwa waathirika hatua
inayolenga kuwapa pole waathirika hao.
Alisema
kuwa hatua hizo zinalenga kutoa huduma kwa wananchi wengi kuliko kutoa
msaada kwa mtu mmoja mmoja. Alisema wanaotaka kumlaumu Rais basi
wangemlaumu kama angekuwa Serikali yake haijatoa huduma hizo muhimu.
Alipoulizwa
kuhusu kauli hizo za Mbowe, Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO
ambaye pia ndiye Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbasi alisema
lugha ya Rais na Serikali kwa ujumla kuhusu maafa ya Kagera na mengine
yaliyotokea nchini haijawahi kubadilika wala kutetereka.
“Rais
na Serikali yake kwa ujumla wamekuwa wazi katika hili na itaendelea kuwa
wazi kwamba kama Taifa hatuna raslimali za kumsaidia kila mwathirika wa
tetemeko la Kagera kwa kumfanyia kila kitu.
Serikali
ilitibu majeruhi wote bure, ilisaidia kifuta machozi kwa familia zote
zilizopoteza ndugu zao, ilisaidia waathirika kupata huduma za kibinadamu
kama dawa, ushauri wa kisaikolojia, vyakula na mavazi na maturubai kwa
makazi ya muda na inaendelea kujenga miundombinu kama shule, zahanati na
barabara,” alisema.
Dkt
Abbas akasisitiza: “Mbowe atafute tu ajenda nyingine. Nilikwenda Kagera
na kukaa kwa wiki mbili baada ya tetemeko kutokea ambapo nilibahatika
kuzungumza na waathirika mijini na vijijini; hakuna kati yao popote
aliyekuwa anasema Serikali itamjengea nyumba au kumsaidia kila kitu. Kwa
hiyo ujumbe wa Rais ulieleweka tangu mwanzo na hata sasa.”
Ameongeza kuwa Serikali imesaidia kaya maskini kwa kuwapatia sajuri na mabati kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
No comments:
Post a Comment