WAHARIRI WAKUTANA KUPITIA SHERIA YA HUDUMA YA VYOMBO VYA HABARI ILIYOPITISHWA NA BUNGE
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia),
akizungumza Dar es Salaam leo wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa
wahariri kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari uliyopitishwa na
Bunge pamoja na kujadili mpango mkakati wa TEF wa kuendeleza tasnia ya
habari nchini. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile na
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
Mtaalamu Mshauri Rosemary Mwakitwange akiongoza
mkutano huo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura.
Mwakilishi kutoka Jukwaa la Wahariri la Afrika Kusini akizungumza kwenye mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa TEF, Deodatus Balile akizungumza kwenye mkutano huo.
Mwenyekiti
wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Theophil Makunga (kulia) na
Mtaalamu Mshauri Rosemary Mwakitwange wakiangalia mada zitakazo jadiriwa
katika mkutano huo.
Wahariri Idrisa Jabir na Charles Mwankenja (kulia), wakijadili jambo.
Wahariri
kutoka kushoto, Joseph Kulangwa, Abdallah Majura na Ibrahim Issa ambaye
ni mjumbe wa TEF wakifurahia jambo kwenye mkutano huo.
Wahariri wakifurahia jambo.
Wahariri wakiwa kwenye mkutano huo.
Wahariri, Joseph Kulangwa na Abdallah Majura wakipitia mada zitakazo jadiriwa.
Wahariri, Shermax Ngahemera (kushoto), Julian Msacky na Flora Wingia (kulia), wakifuatilia mada za mkutano huo.
Taswira ndani ya ukumbi wa mkutano huo
Wahariri ndani ya chumba cha mkutano.
Na Dotto Mwaibale
WAHARIRI
wa vyombo vya habari wamekutana katika mkutano maalumu wa siku mbili
kwa ajili ya kujadili mambo kadhaa yanayohusu tasnia hiyo nchini.
Akizungumza
wakati akifungua mkutano huo Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF) Theophil Makunga alisema mkutano huo utawajumuisha wadau wa sekta
ya habari kutoka ndani na nje ya nchi.
"Tumewaalika wenzetu wa nje ili watupe uzoefu wa jinsi wanavyofanya katika tasnia ya habari katika nchi zao" alisema Makunga.
Alisema
katika mkutano huo ambao unafanyika Hoteli ya Protea Court Yard mambo
yatakayo zungumziwa ni kupitia sheria ya huduma ya vyombo vya habari
iliyopitishwa na Bunge na kusainiwa na Rais Dk. John Magufuli pamoja na
kujadili mpango mkakati wa Jukwa la Wahariri wa kuendeleza tasnia ya
habari nchini.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura alisema ni
muhimu kwa wanahabari kuwa na mpango mkakati wa miaka 10 ili kupata
majibu sahihi ya tasnia hiyo.
No comments:
Post a Comment