Header Ads

Vyuo India vyaeleza vinavyoweka ulinzi vyuoni

BAADHI ya maofisa kutoka vyuo vikuu vya India ambao wamekuwa wakishirikishi maonyesho ya vyuo vya nje yaliyofanyika tarehe 14 hadi 15 Desemba Dodoma, wameeleza namna vyuo nchini mwao vinavyoweka kipaumbele katika ulinzi wa wanafunzi wao.

Ofisa kutoka Chuo Kikuu cha Lovely (LPU), Love Kumar alisema, katika maonyesho hayo yaliyoandaliwa na Kampuni ya wakala wa vyuo vya nje, Global Education Link (GEL) kuwa kwa mfano katika chuo chake kuna kamera nyingi zilizofungwa katika maeneo mbalimbali kuchunguza kila kinachoendelea.

“Tunatamani kuona watu wanakuja kwetu na kusoma kwa amani, India ni nchi ya amani. Hata hivyo tumeweka zaidi ya kamera 4000 kuhakikisha kila kitu kinaangaliwa kwa ufasaha” aliongeza Kumar.

Naye Mratibu wa wanafunzi wanaotoka nje kutoka Chuo Kikuu cha Maharishi Markandeshwar, Rashmi Garg alisema hali ni hivyo pia katika chuo hicho. Alifafanua kwamba sababu ya kufunga vifaa vya ulinzi ni kuendelea kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Mojawapo ya majengo ya Chuo Kikuu cha Lovely nchini India. Global Education Link (GEL) ni mwakilishi rasmi wa chuo hiki hapa nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Global Education Link (GEL), Abdulmalik Mollel, aliwahakikisha Watanzania kwamba kampuni yake inafanya inaloweza kuhakikisha Watanzania wengi zaidi wanakwenda nje ya nchi kupata ujuzi ambao watarudi nao nchini kwa ajili ya kusaidia kukuza maendeleo.

No comments:

Powered by Blogger.