Header Ads

WAZIRI PROF.NDALICHAKO AWASILI MKOANI KIGOMA KUKAGUA MIUNDOMBINU YA CHUO CHA ELIMU YA TAIFA WILAYANI KASULU

Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi  akitoa taarifa ya wilaya kwa Waziri
  Waziri Prof.Ndalichako akiwapongeza Viongozi wa Wilaya ya Kasulu kwa kubuni mkakati endelevu wa elimu
 Waziri Prof.Ndalichako na DC Kanali Mkisi wakikagua miundombinu ya Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu
Waziri Prof.Ndalichako akitoa akisisitiza jambo kwa Mkuu wa wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi
 Waziri Ndalichako na Kanali Mkisi wakikagua ufanyaji wa mitihani katika shule ya msingi Mwenge,Wilayani Kasulu mkoani Kigoma

Na Abel Daud-Globu ya Jamii Kigoma

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof.Joyce Ndalichako amewahakikishia wanafunzi kote Nchini kwamba Serikali ya awamu ya tano imejipanga kuhakikisha inatengeneza mazingira rafiki ili kila atakaye faulu aweze kuendelea na hatua ya juu zaidi ya kielimu.

Hayo ameyasema leo hii Wilayani Kasulu alipotembelea Shule ya Msingi Mwenge pamoja na Chuo cha Elimu ya Taifa Kasulu kukagua miundombinu tayari kwa kupokea wanafunzi wa diploma kutoka UDOM.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kasulu Kanali Martin Mkisi amemueleza Waziri Ndalichako kuwa Wilaya yake imejipanga kuinua elimu kwa kiwango kikubwa na kuwataka watumishi wa halmashauri za Kasulu pamoja na wananchi kwa ujumla kumpa ushirikiano ili kufikia malengo waliyojipangia ya kuinua elimu wilayani hapo.

Prof.Ndalichako ameupongeza uongozi wa Wilaya ya Kasulu kwa kubuni mkakati endelevu wa kuinua elimu wilaya ya kasulu na kuwataka kusimamia swala hilo kwa vitendo.

No comments:

Powered by Blogger.