KAMPUNI YA ASAS IRINGA YAPONGEZWA KWA KUJITOLEA MIRADI YA ZAIDI YA TSH MILIONI 400 HOSPITALI YA MKOA
Na MatukiodaimaBlog.
SERIKALI ya mkoa wa Iringa imepongeza msaada mkubwa uliotolewa na kampuni ya Asas ya mkoa hapa wa ujenzi wa jengo la kituo cha damu salama cha kisasa na ujenzi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti katika Hospitali teule ya mkoa wa Iringa pamoja miradi itakayogharimu zaidi ya Tsh milioni 400
Katika taarifa iliyosomwa na mganga mkuu wa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa Dr Robert salim wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika miradi hiyo leo mbele ya mgeni rasmi mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza alisema kuwa awali uongozi wa hospitali hiyo ulimwandikia barua mfanyabiashara huyo ili kusaidia msaada wa kontena ambalo lingetumika katika kituo cha benki ya damu salama ila mfanyabiashara huyo alijitolea kujenga jengo hilo la kisasa na kuongeza msaada wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti .
“Kutokana na agizo la Serikali la kuanzisha Benki za damu salama katika Mikoa..... Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Mfadhili Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS iliona ni vyema kujenga jengo la Kituo Kidogo cha damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ili kufikia azma hiyo. ...Hospitali ilimuomba Mfadhili huyo atoe msaada wa “Container” kwa ajili ya shughuli hiyo, lakini Mfadhili kwa kuona umuhimu wa huduma ya damu salama katika Mkoa aliomba apewe ramani ili ajenge kituo hicho badala ya kutumia“Container”.”alisema
Dr Salim alisema kuwa Hospitali hiyo kabla ya mfanyabiashara huyo kujitolea ujenzi wa jengo hilo kituo cha kidogo cha damu salama ulikuwa ukitegemea damu kutoka kituo cha kanda kilichopo mkoani Mbeya ila sasa wataweza kukusanya damu kupitia kituo hicho.
Alisema kuwa lengo la mradi huu ni Kuboresha upatikanaji wa huduma za damu salama katika Mkoa wa Iringa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya damu salama katika Vituo vya kutolea huduma za afya na kupunguza vifo vya Uzazi, Watoto wachanga, Watoto na Wahanga wa ajali za barabarani na kuwa lengo la Mkoa kwa mwezi ni kukusanya chupa 784 na kwa mwaka ni chupa 9,413 (units).
Hata hivyo alisema mahitaji ya damu kwa mwezi katika Mkoa ni chupa 700 (unit) na katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ni chupa 160-200 Units kwa mwezi kuwa tangu kituo kianze kutumika mwezi Februari,2016 Mkoa umekusanya chupa 2,065 (22%) hadi sasa.
“Tunakushukuru mkuu wa mkoa kwa kukubali mwaliko wetu wa kuwa Mgeni Rasmi katika hafla hii ya kuweka mawe ya msingi katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Mfadhili wetu Salim F. Abri Mkurugenzi wa Kampuni ya ASAS ya Iringa. Katika hafla hii fupi tutakuomba uweke jiwe la Msingi katika Mradi wa jengo la Kituo Kidogo cha Damu Salama na Jengo la Wodi ya Watoto wachanga vyote vikiwa ni hisani kutoka kwa mfadhili wetu Salim F Abri “
Alisema kuwa ujenzi huo unafanywa namkandarasi anayenga mradi huu ni Buyungu General Enterprise wa Iringa chini ya usimamizi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambaye amechangia kuchora ramani za jengo hili na kusimamia mradi mpaka ulipokamilika, mchango wake kama angelipwa ni Tshs.13,939,200.00.
Na kuwa utekelezaji wa mradi ulianza kutekelezwa mwezi Novemba, 2014 na umekamilika mwezi Agosti, 2015. Jengo limeanza kutumika mwezi Februari, 2016. Pamoja na kujenga jengo hili Mfadhili pia ametoa msaada wa samani, mafriji makubwa 4 ya kutunzia damu na Computer 1 wenye thamani ya Tshs.30,000,000.00.
`
Aidha, Hospitali ya Vicenza ya Nchili Italia ilichangia Tshs. 800,000.00 kwaajili ya kusafisha eneo la ujenzi na Meneja wa Benki ya Damu Salama ya Kanda Mbeya ametoa msaada wa Vitanda 2 vya kutolea damu, Mizani (weighing scales) za kupimia uzito chupa za damu na Mzani 1 wa kupimia watu wanaojitolea damu.
Alisema Mpaka umekamilika mradi huu wa kituo cha damu salama umegharimu jumla ya Tshs.154,880,000.00 bila samani na vifaa tiba kuwa faida kuwa ya mradi huo uboresha utoaji wa huduma za damu salama kwa kuwa na eneo kubwa la kufanyia kazi,Kupunguza malalamiko ya wananchi kwa kukosa damu salama.
Pia Kuzuia maambukizi ya magonjwa ya VVU/UKIMWI, Hepatitis B na C na Kaswende,Kupunguza vifo vya uzazi, watoto wachanga, watoto na wahanga wa ajali vinavyotokana upungufu wa damu au kutokwa na damu nyingi,Kupunguza gharama za kufuata damu salama umbali mrefu (Damu salama Kanda Mbeya) na kuongeza kuwa Wanufaika zaidi ni
Watoto, Watoto wachanga, Mama wajawazito, Wahanga wa ajali za barabarani na jamii kwa ujumla.
Dr Salim alisema kupitia mradi huo wanategemea Kupunguza malalamiko ya wananchi juu ya huduma isiyoridhisha ya damu salama katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa na Halmashauri na kukomesha tatizo la rushwa.
Kuhusu mradi wa jengo la watoto wanaozaliwa njiti alisema kuwa Mpaka utakapokamilika mradi huu unatarajiwa kugharimu jumla ya Tshs.309,210,000.00 bila samani na vifaa tiba ambazo zote fedha za mfadhili huyo kampuni ya Asas.
Akizungumzia hatua ya familia yake kujitolea kujenga miradi hiyo mikubwa Asas alisema ni kutokana na changamoto kubwa aliyoiona baada ya kutembelea Hospitali hiyo na hata mmoja kati ya wanafamilia wake kupoteza mtoto baada ya kuzaliwa njiti na kukosa chumba kwa ajili ya kunusuru uhai wake.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza pamoja na kupongeza kampuni ya Asas kwa kujitolea misaada hiyo bado aliomba wahisani wengine kuzidi kujitolea kwa ajili ya maendeleo na kuwa kama mkoa unatambua mchango mkubwa wa kimaendeleo unaofanywa na kampuni ya Asas pia mfanyabiashara Rajan aliyepata kujitolea kujenga chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo .
Awali mkuu wa wilaya ya Iringa akimkaribisha mkuu wa mkoa kuweka mawe ya msingi katika miradi hiyo alisema misaada anayoendelea kutoka Asas si tu kwa CCM na serikali yake ila hata kwa vyama vya upinzani na wakazi mbali mbali wa mji wa Iringa hivyo kutaka Halmashauri ya Manispaa kutunza miradi hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza (kushoto) akimpongeza Salim Asas (kulia) mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika miradi mikubwa miwili iliyofadhili kampuni ya Asas ukiwemo mradi wa jengo la kituo cha damu salama Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa na jengo la watoto wanaozaliwa njiti yote yaliyofadhiliwa kwa zaidi ya Tsh milioni 400 na kampuni hiyo ya Asas ya mkoa wa Iringa(picha na matukiodaimaBlog ) |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akisaini kitabu cha wageni |
Mkurugenzi wa kampuni ya Asas ya Iringa wa tatu kushoto akiwa katika Hafla hiyo |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akitoa hutuba yake ya ufunguzi wa miradi hiyo |
Damu iliyochangiwa |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza akizindua majengo hayo kwa hotuba |
Mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na mfadhili wa miradi ya jengo la Benki ya damu na jengo la watoto njiti wakiweka jiwe la msingi leo anayeshuhudia ni mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela |
Mkuu wa mkoa wa Iringa akiwa ndani ya jengo la benki ya damu |
Viongozi mbali mbali wakiwa na mkuu wa mkoa kukagua kituo hicho |
No comments:
Post a Comment