RAIS MSTAAFU DK JAKAYA KIKWETE AONGOZA MAMIA MAZISHI YA BI SHAKILA, MBAGALA CHARAMBE JIJINI DAR LEO.
s
Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete akiweka udongo kwenye kaburi la
Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake Mbagala
Charambe,jijini Dar .
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiweka udongo
kwenye kaburi la Bi Shakila Said,wakati wa maziko huko nyumbani kwake
Mbagala Charambe,jijini Dar.
Makamu
wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan akiweka saini kitabu cha maombolezo
cha Bi Shakila Mbagala Charambe,jijini Dar,kushoto ni Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye.
Mke
wa Rais Mstaafu awamu ya nne,Mama Salma Kikwete akiweka saini kitabu cha
maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwake Mbagala
Charambe,jijini Dar.
Rais
Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa pili kulia) na Waziri wa
Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye (pili kushoto)
wakishiriki maziko ya aliyekuwa Mkongwe,mwimbaji mahiri wa muziki wa
Taarabu hapa nchini,Bi Shakila Saidi ambaye mazishi yake yamefanyika leo
huko nyumbani kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Makamu
wa Rais Mh,Samia Suluhu akijadiliana jambo na mmoja wa waombolezaji
nyumbani kwa marehemu,kabla ya maziko kufanyika.Bi Shakila,amefariki
ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe.
Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye akiwa na baadhi ya
waombolezaji wengine wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya na
wanamuziki wakongwe wakiwa kwenye mazishi ya Bi Shakila,hukko nyumbani
kwake Mbagala Charambe,jijini Dar.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye mazishi ya Bi Shakila,aliyefariki ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe.
Baadhi ya Waombolezaji wakiwa nyumbani kwenye mazishi ya Bi Shakila,aliyefariki ghafla nyumbani kwake,huko Mbagala Charambe.
Mwili wa marehemu Bi Shakila ukiswaliwa tayari kwa maziko
Waombelezaji
wakiwa wamebeba Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Bi Shakila
wakielekea mazikoni,jioni ya leo huko nyumbani kwake Mbagala
Charambe,jijini Dar.
Mwili ya Bi Shakila tayari umeishapumzishwa kwenye nyumba yake ya Milele
Safari ya mwisho ya Bi Shakila Said .
Rais
Mstaafu awamu ya nne,Dkt Jakaya Kikwete (wa tatu kulia) akijalidiliana
jambo na Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mh.Nape Nnauye
(pili kushoto).
Baadhi
ya wanamuziki wakongwe na bongofleva wakiwa katika picha ya pamoja mara
baada ya kushiriki mazishi ya Bi Shakila huko nyumbani kwake Mbagala
Charambe jijini Dar
Rais Mstaafu awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete akizungumza na waombolezaji.
Katibu MKuu wa Shirikisho la Wanamuziki nchini,John Kitime akiweka saini kitabu cha maombolezo cha Bi Shakila Said ,huko nyumbani kwa marehemu Mbagala Charambe,jijini Dar.
No comments:
Post a Comment