Header Ads

MBUNGE MAHAMOOD MGIMWA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA MUFINDI KASIKAZINI

post-feature-image
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo

 
Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikagua baadhii ya maeneo ambapo michezo hiyo itafanyika


na fredy mgunda,iringa. 

Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa ameweza kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu  za Jimbo hilo huku akitaka michezo yote kuendelezwa.

Mgimwa ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.

Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mgimwa amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni  kutokana na ahadi yake  yeye ka,a Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku  baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.

“Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata. Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mgimwa.
Mgimwa ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge.
Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi  na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu.
 
Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.
KAWAIDA. MBUNGE MAHAMOOD MGIMWA AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA MUFINDI KASIKAZINI Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu akiwa sambamba na mwenyekiti wa ccm wilaya ya mufindi Yohanes Kaguo Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa akikagua baadhii ya maeneo ambapo michezo hiyo itafanyika na fredy mgunda,iringa. Mbunge wa Mufindi Kusini Mahamood Mgimwa ameweza kugawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo huku akitaka michezo yote kuendelezwa. Mgimwa ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Mufindi Kusini katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni. Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mgimwa amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye ka,a Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza. “Niliahidi kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata. Lakini pia mimi mwenyewe niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.” Alieleza Mgimwa. Mgimwa ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi zake kama Mbunge. Amesema kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya. Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi na mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya mpira wa miguu. Aidha, amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.

No comments:

Powered by Blogger.