Header Ads

wengine 10 waibuka milionea droo ya 5 ya tusker fanya kweli Na uwini.


Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Juhudi Ngolo(kushoto) akihakiki taarifa za moja ya mshindi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko kwa Wateja kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Lulu John Mduma(kulia)
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko kwa Wateja kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Lulu John Mduma akiongea kwa njia ya simu na mmoja wa washindi wa droo ya tano ya Tusker Fanya Kweli Uwini
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko kwa Wateja kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Lulu John Mduma akitoa ufanunuzi zaid wakati wa droo ya tano ya Milioni 100 na Tusker Fanya Kweli Uwini
Meneja Rasilimali Watu wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Paul Hamidu Kimasharo(kushoto) akichezesha droo ya tano ya Tusker Fanya Kweli Uwini huku akishuhudiwa na Afisa Mkaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini Juhudi Ngolo(wa pili kushoto) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Masoko kwa Wateja kutoka Kampuni ya Bia ya Serengeti Lulu John Mduma(wa pili kulia) na mtangazaji wa ITV Abdallah Mwaipaya(kulia).

                                                                                                                                                  
Promosheni ya aina yake inaendelea huku watanzania wengi zaidi wakibadilisha maisha yao.

27 Juni, 2016: Baada ya kutoa washindi ishirini kwa mara moja wiki iliyopita jana kupitia promosheni inayoendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti ijulikanayo kama Tusker Fanya Kweli Uwini imeendelea huku washindi wengine kumi wakipatikana katika droo ya tano ya promosheni hiyo kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini. Washindi hao wanafanya jumla ya idadi yote kufikia washindi sitini mpaka sasa waliojipatia Milioni moja kila mmoja. 
 
Katika kampeni hii inayoendelea ya Tusker Fanya Kweli Uwini tayari washindi 50 walikabidhiwa fedha zao katika hafla za makabidhiano zinazofanyika kila wiki. Washindi wote ambao tayari wameshapokea pesa hizo wameshuhudia kupokea pesa zao kwa utaratibu mzuri. Million 60 tayari zimeshaenda kwa washindi wa promosheni hiyo, bado Milioni 40 kushindaniwa.

Droo hiyo ya 5 iliyofanyika katika studio za ITV jana, ilirushwa kupitia televisheni hiyo, huku ikishuhudiwa na Afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini na wadau wengine nao walishuhudia kwa umakini kila droo ilivyofanyika na uhalisia wake. Wafuatao walitangazwa kuwa washindi wa droo ya 5; Fatma Abuu kutoka Morogoro, Hassan Rajabu kutoka Dodoma, Patrick Kimaro na Philiasi John kutoka Mwanza, Bakari Rashidi anayetoka katika mkoa wa Pwani, Lucy J.Mosile pamoja na Deodatus John kutoka Dar es salaam. 
 
Washindi wote waliopatikana walikuwa na shauku ya kueleza jinsi walivyoingia katika mashindano na jinsi watakavyotumia pesa hizo walizopata. Washindi wote walipewa maelekezo ya kufika katika hafla ya makabidhiano na jinsi ya kupata pesa zao tayari kwa kuanza safari ya umilionea.

No comments:

Powered by Blogger.