KAMPUNI YA NEXGEN YALETA WANAFUNZI WA AUSTRALIA KWAAJILI YA KUTOA MAFUNZO YA KUMLINDA MTOTO.
KAMPUNI
ya Nexgen inayojishughulisha na utetezi wa Haki za watoto hapa nchini
wamewapokea wanafunzi 21 wa shule ya All Saints Anglican ya nchini ya
Australia.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob
Kahemele mara baada ya kuwapokea wanafunzi 21, wazazi wawili na walimu
wawili wa shule ya All Saints Anglican ya nchini ya Australia amesema
kuwa wamekuja kwaajili ya kutoa mafunzo mbalimbali kwaajili ya kumkinga
mtoto wa kike ili aweze kuwa salama na kubaki salama.
Amesema
kuwa nchi ya Australia ndio nchini inayoongoza katika kumlinda mtoto na
kuepukana na matatizo mbalimbali yanayomkumba mtoto wa kike hasa
matatizo ya kubakwa kutokana na kesi nyingi kujitokeza hapa nchini Pia
amewaasa viongozi wa nchi waongeze nguvu juu ya kumlinda mtoto.
Kahemele
amesema kuwa viongozi wa siasa waachane kuzungumza vitu visivyo vya
msingi bungeni na adala yake waanze kufikilia juu ya kumlinda mtoto hasa
wa kike ili kuepukana na matatizo mbalimbali yanayomkumba.
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob Kahemele
akizungumza jambo na walimu wa shule ya All Saints Anglican ya nchini
Australia mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Mwalimu
Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi
Mtendaji wa kampuni ya Nexgen, Jacob Kahemele akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya wanafunzi wa shule ya All Saints Anglican
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam. Amesema kuwa wanafunzi hao wamekuja hapa nchini kwaajili ya
kusaidi na kuhamasisha jamii kuzuia na kupambana juu ya usala wa mtoto
katika maisha yake ya utoto.
Mwalimu
wa shule ya All Saints Anglican ya nchini Australia, Blendan Collaghan
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mala baada ya
kuwasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
Salaam jana.
Wanafunzi wa Shule ya msingi ya Fountain Gate Academy wakiwapokewa
na kuwafunga skafu za bendera ya Taifa wanafunzi wa shule ya All Saints
Anglican ya nchini ya Australia walipowasili katika uwanja wa ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana.
No comments:
Post a Comment