SERIKALI NA TTCL KUMILIKI KWA PAMOJA MKONGO WA TAIFA WA MAWASILIANO.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, akiweka
saini kitabu cha Wageni alipotembelea ofisi za Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL) Mkoa wa Kigoma.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoani Kigoma
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea ofisi hizo.
Baadhi
ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Mkoani Kigoma
wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa (hayupo pichani) alipotembelea ofisi hizo.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (aliekaa
katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi wa TTCL Kigoma
alipotembelea ofisi hizo. Wengine waliokaa kutoka kushoto ni Meneja wa
TTCL Kigoma, Bw Lugage Abdallah, Kaimu Mkuu wa Mkoa Kigoma, Bw Saveli
Maketa, Mbunge wa Kigoma Mjini Zito Kabwe na Afisa Mtendaji Mkuu wa
TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura.
SERIKALI
kwa kushirikiana na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), zitamiliki kwa
pamoja Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) ili kuongeza ufanisi wa
mkongo huo katika kutoa huduma za mawasiliano nchini.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Profesa Makame Mnyaa Mbarawa
amesema, Serikali ipo tayari kushirikiana na kampuni ya TTCL katika
kuumiliki Mkongo huo kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na TTCL tangu
mwaka 2010 ilipopewa jukumu la kuujenga, kuusimamia na kuuendesha Mkongo
huo.
Waziri
Mbarawa ametoa kauli hiyo alipotembelea Ofisi za Kampuni ya Simu TTCL
Mkoa wa Kigoma ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku 5 Mkoani humo
kukagua shughuli za Taasisi zilizo chini ya Wizara yake.
Mhe
Mbarawa alisema, Ombi lililotolewa na TTCL la kumiliki mkongo lina
mantiki kubwa kutokana na uwezo wa kiufundi, kitaalamu na kiundeshaji
uliopo ndani ya kampuni hiyo lakini kutokana na Sababu za kiserikali, ni
lazima Serikali ibaki kuwa na mkono wake ndani ya Mkongo ili
kuudhibiti, kuulinda kuhakikisha kuwa unatumika kwa tija na kufanya kazi
zake kwa ufanisi.
"Tutaendelea
kuzungumza Serikalini ili tukubaliane mgawanyo wa asilimia katika
Mkongo wa NICTBB. Sina tatizo kuipa Ttcl asilimia hadi 70 na Serikali
ibaki na asilimia 30. Cha msingi hapa ni kwamba lazima Mkono wa Serikali
uwepo.. Huu ndio msimamo wangu kwa sasa, tutaendelea kujadiliana ili
tuwe na namna bora zaidi ya kutekeleza mpango huu. Nia yangu na wenzangu
wote Wizarani na Serikalini kwa ujumla, ni kuhakikisha Ttcl inaimarika
na kuwa kinara katika huduma za Mawasiliano nchini" amesisitiza Mhe
Mbarawa.
Akichangia
hoja hiyo, Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT, Wazalendo), Mhe Zito Kabwe
alieongozana na Waziri Mbarawa katika ziara hiyo alisema, TTCL imeonesha
uwezo mkubwa na jitihada za dhati tangu ujenzi hadi kuuendesha Mkongo
kwa niaba ya Serikali na kushauri kuwa, wakati umefika kwa TTCL
kukadhiwa mamlaka ya miundombinu hiyo ili kuipa TTCL nguvu zaidi na
uhuru katika kuendesha chombo hicho.
"...Kwa
maoni yangu, TTCL inastahili kukabidhiwa Mkongo wa NICTBB, wakipata
mkongo huu wataimarika sana. Nimekuwa nikishauri mara zote kuwa,
tukikabidhi Mkongo kwa TTCL tunaweza hata kuwapa jukumu moja tu la
kufanya biashara ya Data, wakaachana na biashari nyingine ili waendeshe
Mkongo kwa ufanisi" amesema Mhe Zito.
Kwa
Upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dk. Kamugisha Kazaura alisema,
kampuni ya TTCL inaishukuru Serikali kwa nia njema ya kutaka
kuimilikisha kampuni hiyo sehemu ya Mkongo kwa kuwa ni jambo lenye tija
kibiashara na kuthamini juhudi kubwa na moyo wa uzalendo ulioneshwa na
Wafanyakazi wa TTCL katika kuujenga na kuuhudumia Mkongo tangu
kuanzishwa kwake.
Awali,
Katika taarifa yake kwa Mhe Waziri, Meneja wa TTCL Mkoa wa Kigoma, Bw
Lugage Abdallah alisema, Kampuni hiyo imejipanga kuongeza ufanisi kwa
kuboresha huduma, kuongeza idadi ya Wateja na kutatua kwa haraka
matatizo ya kiufundi yanapojitokeza ili kuwapa wateja huduma za uhakika.
"Mhe
Waziri, tunakabiliwa na changamoto kubwa ya Uharibifu wa Miundo mbinu ya
TTCL na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano. Tunashirikiana na jamii na
vyombo vya Ulinzi na Usalama kulinda miundo mbinu yetu na juhudi
zimeanza kuzaa matunda kwa kukamata Wahalifu. Ombi letu kubwa kwako ni
kuisaidia TTCL hasa katika kupata malipo ya huduma tunazotoa kwa Taasisi
za Umma ambazo zimekuwa ni wadaiwa sugu" alisema Bw Abdallah.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano amekamilisha ziara yake Mkoani
Kigoma Jumamosi Aprili 02 na kuelekea Mkoani Katavi kwa ziara kama hiyo
No comments:
Post a Comment