RAIS WA RT,ANTHONY MTAKA AULA SHIRIKISHO LA RIADHA LA DUNIA (IAAF)
Rais
wa Shirikisho la Riadha Duniani (IAAF) Lord Sebastian Coe (kushoto)
akipeana mkono na Rais wa Shirikisho la riadha Tanzania (RT) Anthony
Mtaka. Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
SHIRIKISHO
la mchezo wa Riadha Duniani (IAAF) limemteua Rais wa Shirikisho la
Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka kuwa miongoni mwa wajumbe wanaounda
kundi la ushauri wa mikakati ya mawasiliano la shirikisho hilo.
Rais
wa IAAAF ,Lord Sebastian Coe alitangaza uteuzi huo hivi karibuni ambapo
wajumbe wengine ni Abrahamson Alan wa Marekani, Rodan Joe Junior ,Sierra
Calixto ,,Karamarinov Dobromir kutoka Bulgaria na Rochdi Souad wa
Ufaransa.Akizungumza kuhusu uteuzi huo Mtaka ambaye pia ni mkuu wa mkoa
wa Simiyu alisema amepokea uteuzi huo kwa furaha kutokana na kuwa ni
nafasi ya juu katika sekta maarufu ya michezo katika ngazi ya
kimataifa.
“Nimefurahishwa
na uteuzi huu hasa ukizingatia nimeteuliwa nikiwa rais wa shirikisho la
riadha mwenye umri mdogo kuliko wote kwa sasa takuwa na fursa ya
kujifunza mambo mengi mazuri.”alisema Mtaka.
Alisema
uteuzi huo ni faida kubwa kwa maendeleo ya michezo katika taifa letu,
hasa kipindi hiki ambapo serikali ya awamu ya tano inapoandaa mkakati wa
kuiweka sekta ya michezo kuwa sehemu kubwa ya ajira.
Mtaka
alisema Tanzania itapata nafasi pana zaidi ya kuwakilishwa katika
mikutano mikubwa ya mchezo wa riadha duniani (Decision Making) eneo
ambalo linatoa fursa kubwa kwa maandalizi ya mashindano makubwa yajayo
baada ya mashindano ya Olyimpiki yatakayofanyika katika jiji la Rio de
Jeneiro mwaka huu.
“Taifa
litarajie uwakilishi wenye tija, sababu mimi nimeteuliwa kati ya
wajumbe nane ambao kila mmoja wao anawakilisha eneo kubwa, hivyo kama
nimepewa dhamana ya kuiwakilisha bara zima la Africa, kwa vyovyote
nitaweka maslahi ya nchi yangu mbele bila kuathiri utendaji wa jukumu
nililopewa.”alisema Mtaka.
“
Uteuzi wangu ni sifa kwa taifa zima, sifa ambayo itafufua mtazamo mwema
ulioonyeshwa na wanariadha wakongwe walioiletea taifa sifa kama Filbert
Bayi, Suleiman Nyambui, Gidamis Shahanga, Juma Ikangaa bila kumsahau
Mzee John Stephen Akhwari aliyeshiriki Mexico City Games 1968.”aliongeza
Mtaka.
Aidha
Mtaka alisema uteuzi huo umeongeza hamasa ya kuwekeza maradufu katika
kambi ya timu ya taifa ya riadha iliyopo katika hosteli ya Chuo cha
misitu cha FITI kilichopo West Kilimanjaro wilayani Siha na Arusha.
No comments:
Post a Comment