Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla azindua rasmi jengo jipya la taasisi ya T-MARC Tanzania
TAASISI
isiyo ya kiserikali T-MARC Tanzania imezindua rasmi jengo lake jipya
pamoja na ghala maalum la kisasa litakalotumika kuhifadhia bidhaa zao
ikiwemo zile za mipira ya kiume na kike kupitia bidhaa zao za DUME.
Tukio hilo limefanyika rasmi mapema jana Aprili 1.2016, ambapo
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Andrea Kigwangalla alikuwa mgeni rasmi akiwakilisha Serikali
katika tukio hilo kubwa na la kihistoria.
Akizungumza na wanahabari, Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla
amebainisha kuwa, Serikali inapongeza juhudi za Taasisi za watu binafi
ikiwemo T-MARC Tanzania wanavyofanya juhudi kubwa hapa nchini katika
kuwafikia wananchi kupitia bidhaa zao hizo za kinga.
Dk. Kigwangalla amewapongeza kwa hatua hiyo tokea walipoanza hapa
nchini kuanzia mradi hadi taasisi ambapo kwa hatua yao hiyo pia
imesaidia na mapambano ya virusi vya UKIMWI kwani kupitia bidhaa zao
hizo za kondomu kupitia kondomu za DUME zimekuwa msaada mkubwa sana kazi
hizo wanazofanya wanaisaidia Serikali kwa kiwango kikubwa sana.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc Tanzania, Bi.Diana
Kisaka alishukuru Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na taassi hiyo
kwani imeweza kutimiza malengo yake hapa nchini na itaendelea
kushirikiana na Serikali bega kwa bega kwa kipindi chote.
Aidha, aliongeza kuwa, wataendelea kutoa huduma bora hiyo ya kinga
kupitia bidhaa zao za mipira ya kinga yaani kondomu za DUME ilikuzuia
mapambano ya virusi vya UKIMWI hapa nchini.
Awali Dk. Kigwangalla alipata wasaha wa kukagua mabanda ya
maonyesho ya miradi mbalimbali ya taasisi hiyo na kupata maelezo ya kwa
kina kisha alipata wasaha wa kufungua rasmi jengo hilo la kisasa ambalo
ni la ofisi za taasisi hiyo pamoja na kuzindua ghala maalum la
kuhifadhia bidhaa hizo za DUME Condom.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Andrea Kigwangalla akisalimiana na Mkurugenzi mtendaji wa T-Marc
Tanzania, Bi.Diana Kisaka wakati wa kuwasili katika eneo la tukio hilo
la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania
yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akisalimiana na Mjumbe wa bodi ya T-MARC
Tanzania, Bi Joyce Mhavile wakati wa kuwasili katika eneo la tukio hilo
la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania
yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza Meneja Mradi wa T-MARC
Tanzania, Bi. Halima Mwinyi wakati wa kutembelea miradi ya kwenye
mabanda ya maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la
kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza afisa wa T-MARC Tanzania,
Bi. Sophia Komba wakati wa kutembelea miradi ya kwenye mabanda ya
maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la
makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,
Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla akimsikiliza afisa wa T-MARC Tanzania,
Bi.Doris Chalambo wakati wa kutembelea miradi ya kwenye mabanda ya
maonyesho kwenye tukio hilo la ufunguzi rasmi wa jengo la kisasa la
makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es Salaam.
Jengo jipya la T-MARC Tanzania kabla ya uzinduzi huo linavyoonekana
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Hamisi Andrea Kigwangalla akikata utepe kuashiria kulifungua rasmi jengo
hilo la kisasa la makao makuu ya T-MARC Tanzania yaliyopo Jijini Dar es
Salaam.
No comments:
Post a Comment