MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI (WCF), WATOA ELIMU KWA VIONGOZI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI
Mkurugenzi
Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafnyakazi, WCF, Masha Mshomba, akizungumza
wakati wa semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo kwa viongozi wa
vyama vya wafanyakazi nchini, na kufanyika makao makuu ya Mfuko,
barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam Aprili 19, 2016. Lengo la
semina hiyo ilikuwa ni kutoa elimu kwa viongozi hao juu ya shughuli za
Mfuko na faida ya wafanyakazi kupatiwa fidia endapo patatokea madhara
awapo kazini. Wengine pichani ni mgeni rasmi, Pendo Z.Berege,
(Mwakilishi wa Msajili wa vyama vya afanyakazi na waajiri, na Peter J.
Mbelwa kutoka Mamlaka ya Udhibiti na usimamizi wa sekta ya hifadhi ya
jamii, (SSRA).
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
MFUKO
wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, umeendesha semina ya siku moja kwa
viongozi wa vyama vya wafanyakazi nchini, ili kutoa elimu juu ya
shughuli za Mfuko na wajibu wa waajiri kwa wafanyakazi wao katika
kuwalipia michango ya mwezi.
Semina
hiyo iliyofanyika makao makuu ya Mfuko, barabara ya Bagamoyo jijini Dar
es Salaam, Aprili 19, 2016, ilifunguliwa na mwakilishi wa Msajili wa
vyama vya wafanyakazi na waajiri, Bi.Pendo Z.Berege.Katika hotuba yake,
Bi. Berege alieleza umuhimu wa waajiri kuwalipia michango wafanyakazi
wake kama sheria inavyotaka, ili kuwawekea akiba pindi wapatwapo na
majanga wakiwa kazini.
Mfuko
wa Fidia kwa wafanyakazi ni taasisi ya serikali chini ya Ofisi ya Waziri
Mkuu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa
wafanyakazi No. 20 ya mwaka 2008.Akiwakaribisha wana semina kwenye
semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Msomba alisema, Mfuko
umeamua kuandaa semina hiyo ili kutoa elimu zaidi kwa wafanyakazi na kwa
kutambua kuwa viongozi wa wafanyakazi ndio wadau wakuu wa Mfuko huo,
semina hiyo itawasaidia kujua kazi za Mfuko lakini pia wajibu wa waajiri
kwa wafanyakazi katika kutoa michango ya kila mwezi.
Akitoa
mada juu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, Afisa Uhusiano Mwandamizi
wa Mfuko huo, Sebera Fulgence, alisema, Mfuko huo upo kisheria ili kutoa
fidia kwa wafanyakazi waumiapo kazini.
Naye
Bi.Amina Likungwala kutoka WCF, amesema katika mada yake ya Wajibu wa
Vyama vya Wafanyakazi ambapo alisema, ni wajibu wa vyama kutoa elimu kwa
wanachama wao ambao ni wafanyakazi lakini pia kuwaeleza waajiri umuhimu
wa kutoa michango kwa wakati
Mshiriki
akisoma kijitabu chenye maelezo ya kina kinachofafanua majibu ya
maswali ya mara kwa mara ambayo wadau wanataka kujua kuhusu WCF.
Bi. Pendo Berege, akifungua semina hiyo
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA,
Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo.
Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, SSRA,
Bi.Irene Isaka, akitoa hotuba ya kufunga semina hiyo. Kulia ni
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Masha Mshomba.
Mzee Mchafu Chakoma, mwakilishi wa viongozi wa wafanyakazi akitoa neno la shukrani
Bw. Chakoma (kushoto), akibadilihana mawazo na Bi. Pendo Berege
Bi Amina Likungwala kutoka WCF, akitoa mada kuhusu wajibu wa vyama vya wafanyakazi
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa WCF, Sebera Fulgence, akitoa mada "Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF).
No comments:
Post a Comment