Header Ads

KASESELA AFUNGUA WARSHA YA KUWAWEZESHA WANAFUNZI KUTUMIA KOMPYUTA NA WAVUTI MKOANI IRINGA

Mkuu wa Wilaya Iringa Richard Kasesela amefungua warsha ya kuwawezesha wanafunzi kutumia kompyuta na wavuti (Bring Computer literacy to children in Tanzania), mradi huu wa Global Out reach ulibuniwa na Bwana Mussle ambaye alitembelea Tanzania akimtembelea binti yake aliye kuja kijitlea Iringa (hawa ni raia wa marekani). Mradi huu unafadhiriwa na;

 BENKI KUU YA TANZANIA, ROTARY  INTERNATIONAL, ROMAN CATHOLIC CHURCH IRINGA, ST THOMAS MORE PARISH KICHANGANI, SUNRISE ROTARY USA, BRADENTON ROTARY USA, ST STEPHENS, TTCL

Mradi huu unashirkisha shule 12 Iringa (POMELINI, MAWELEWELE,LUGALO, IRINGA GIRLS, IFUNDA TECH, NYERERE HIGH SCH, BOMALANG'OMBE,IMAGE, MAFINGA, ST JOSEPH, ST MICHAEL na CAGLIERO). Kila shule imepata kompyuta na wamepewa mafunzo, pia wametoa vifaa kwa ajili ya kituo chenye maktaba kilichotolewa kwa hisani ya baba askofu wa Roman Catholic Iringa.
 
Mkuu wa wilaya aliwaasa waalimu wote wa shule za sekondari kuanza kufikiria uwezekano wa kuwa na maktaba ya kompyuta. baada ya zoezi la maabara kwisha na madawati kuptakina shule zote kitakacho fuatia ni kuhakikisha shule zote zinakuwa computarized.

No comments:

Powered by Blogger.