KAMATI YA MISS TANZANIA YAZINDUA MSIMU MPYA WA MASHINDANO YA UREMBO YA MISS TANZANIA 2016 JIJINI ARUSHA
Mkuu
wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi
akikata utepe kuzindua mashindano hayo jijini Arusha. Wanaoshuhudia
tukio hilo ni Mdau wa tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia
anasifika kwa kufanya mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko
katika nyanja mbalimbali kupitia kipindi chake cha 'Mimi na Tanzania',
Hoyce Temu (kulia), Mkurugenzi wa Lino International Agency ambao ni
waandaaji wa shindano la Miss Tanzania, Hashim Lundenga (wa pili kulia)
na Mrembo wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima.
Yamoto Band ikifanya mambo yake jukwaani ndani ya ukumbi wa Triple A jijini Arusha.
Mrembo
wa Taji la Miss Tanzania 2014/2015, Lilian Kamazima akakitambulishwa
ukumbi kwenye uzinduzi wa msimu mpya wa mashindano ya urembo ya Miss
Tanzania 2016.
Mkurugenzi
wa Lino International Agency ambao ni waandaaji wa shindano la Miss
Tanzania, Hashim Lundenga akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa msimu
mpya wa mashindano ya urembo ya Miss Tanzania mkoa wa Arusha. Katikati
ni Mkurugenzi wa Mwandago Investment, Chris Mwandago ambaye ni muandaji
mashindano ya Miss Tanzania Kanda ya Kaskazini, na kulia ni Mdau wa
tasnia ya urembo Miss Tanzania 1999 ambaye pia anasifika kwa kufanya
mambo mengine ya kijamii na kuleta mabadiliko katika nyanja mbalimbali
kupitia kipindi chake cha 'Mimi na Tanzania', Hoyce Temu.
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu ambaye alikua mgeni rasmi akizungumza jambo.
Wadau wa tasnia ya urembo wakifurahia jambo.
Baada
ya kupewa baraka jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari, Sanaa,
Utamaduni na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye, msimu mpya wa mashindano ya
urembo ya Miss Tanzania 2016 yamezinduliwa tena jijini Arusha na Mkuu
wa wilaya ya Arusha Mjini, Fadhili Nkurlu katika ukumbi wa klabu ya
Triple A jijini humo na zifuatazo ni picha za matukio mbalimbali
yaliyojiri katika uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment