WAZIRI MAGHEMBE AMSIMAMISHA KAZI MTENDAJI MKUU WA HUDUMA ZA MISITU TANZANIA ( TFS), WAKURUGENZI WATATU PAMOJA NA WAKUU WA KANDA NCHI NZIMA
Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe (kulia)
akizungumza katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kumsimamisha kazi
Mtendaji Mkuu na Wakurugenzi watatu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
katika ukumbi wa Ngorongoro Makao Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar
es Salaam leo . Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Maliasili na
Utalii Eng. Ramo Makani.
Baadhi ya Waandishi wa habari Waliohudhuria Mkutano huo wa Waziri wa
Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe katika ukumbi wa Ngorongoro Makao
Makuu wa Wizara hiyo Mpingo House Jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Maliasili na
Utalii, Prof.Jumanne Mghembe amemsimamisha kazi
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu nchini, (TFS) Bw.
Juma Mgoo pamoja na Wakurugenzi wawili
wa wakala hiyo ili kupisha uchunguzi kutokana na ukusanyaji usioridhisha wa mapato yatokanayo
na mazao ya misitu.
Prof. Maghembe ametaja majina ya Wakurugenzi hao aliowasimamisha kazi
kuwa ni Mkurugenzi
Rasilimali Misitu, Bw. Zawadi
Mbwambo pamoja na
Kaimu Mkurugenzi wa Mipango na Matumizi endelevu ya Misitu, Bw. Nurdin Chamuya
Wengine waliosimamishwa kazi ni wakuu wa Kanda za Wakala wa Huduma za
Misitu nchi nzima ambao
ni Bw. Hubert Haule wa Kanda ya
Kusini, Bw. Bakari Rashidi wa kanda ya Mashariki, Bw. Shabani Mwinyi Juma wa
kanda ya kati , Emanuel Minja wa kanda
ya Magharibi pamoja na Bw. Bruno wa
nyanda za juu kusini
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari Makao
Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam, Prof. Maghembe amesema hatua hiyo imekuja baada ya kubaini
shehena kubwa za
magogo aina ya mninga katika Mkoa wa Rukwa wilayani Kalambo yakiwa
yamekatwa na kuwekwa ndani ya makontena kule kule ndani ya msitu
pamoja na kutengenezewa nyaraka feki zinazoonesha magogo hayo yanatoka
nchini Zambia tayari
kwa kusafirishwa kupelekwa nchini China lakini hata hivyo baada ya
kubaini wizi huo hakuna hatua yoyote
iliyochukuliwa na Wakala ya Huduma za Misitu Tanzania ( TFS).
Amesema kuwa baada ya
kubaini hivyo usiku wa jana aliweza kupata taarifa kuwa shehena ya Magogo hayo yenye thamani
ya shilingi milioni 500
yaliyotakiwa kupelekwa Makao
makuu ya Wilaya ya Kalambo yamemwagiwa petrol na yamechomwa moto
Aliongeza
kuwa kumekuwa na ubadhilifu unaofanywa
na Maofisa wa ukusanyaji wa maduhuri ya
Serikali yanayotokana na rasilimali za misitu katika Mikoa na Wilaya kwa
kutowasilishwa katika mfuko Mkuu wa Serikali.
Kwa
upande mwingine , Prof Maghembe amesema kuwa
pesa zitokanazo na makusanyo hayo zimekuwa hazipelekwi benki kwa wakati na hata zikipelekwa
benki zimekuwa zikipelekwa pungufu na
muda mwingine pesa hizo zimekuwa hazipelekwi kabisa.
Wakati
huo huo, Waziri
Maghembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Wanyamapori wa Matumizi Endelevu, Dkt. Charles Mulokozi kwa kosa la
kukaidi agizo la kusaini
vibali vya kusafirisha Wanyamapori nje
ya nchi.
Hatua hiyo imekuja baada
ya jana nyani 61 kukamatwa katika
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na kubaini kuwa Idara ya
Wanyamapori ndio iliyotoa vibali vya
kusafirisha nyani hao na vibali hivyo vikiwa vimetiwa saini na Mkurugenzi huyo.
Ameongeza kuwa ndege ya
kutoka Ulaya Kusini iliyotakiwa
kusafirisha nyani hao imeshikiliwa pamoja na rubani wake kwa mahojiano zaidi.
No comments:
Post a Comment