TAASISI YA WIPA YAJA NA SULUHISHO UWAJIBIKAJI KATI KUPUNGUZA MIGOGORO KATI YA SERIKALI NA WANANCHI
Mkurugenzi Mtendaji wa
Taasisi ya Wajibu, Ludovick Utouh akizungumza na wadishi wa habari jijini
Dar ers Salaam jana.Kushoto ni Afisa mahusiano Hassan Kisena.
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SERIKALI imekuwa ikilalamikiwa na
wananchi kwa kutowajibika ipasavyo kwenye matatizo yao kutokana na kutokuwepo kwa kiunganishi cha
moja kwa moja kati ya wawakilishi na wanaowakilishwa.
Hayo amesema leo Afisa Mtendaji Mkuu
wa Taasisi ya Fikra ya Uwajibikaji Nchini (WIPA), Ludovick Utouh wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, amesema kuwa kutokana
na kiunganishi nchi nyingi zimeingia katika migogoro kati ya wananchi na
serikali zao yanayosababishwa na maamuzi ambayo yanaathiri maisha yao.
Amesema kuwa kuwa taasisi hiyo
imeanzishwa kwa ajili ya masuala ya uwajibikaji na utawala bora kwa kufungua
mlango utakaochochea na kuongeza uelewa mpana wa dhana ya uwajibikaji na
utawala bora nchini.
“Kuwezesha Wananchi Kushiriki Kikamilifu
Kwenye Masuala ya Uwajibikaji na Utawala Bora Katika Usimamizi wa
Rasilimali za Umma” amesema Utouh. Amesema
uhamasishajRi wa wananchi kwenye ushiriki katika masuala ya uwajibikaji
na utawala bora ni jambo la
msingi katika kuhakikisha
maendeleo yaliyopatikana katika
utekelezaji wa dhana hii yanakuwa
endelevu.
Aidha amesema jitihada za kuimarisha uwajibikaji nchini
zilitaachiwa Bunge na taasisi za usimamizi za serikali peke yao, uwezekano wa
kufanikisha utekelezaji huu utakuwa ni
mdogo kwa sababu
suala la uwajibikaji
linahitaji ushiriki wa
wadau mbalimbali ili kuleta tija kwa taifa.
Ludovick Utouh Mdhibiti na mkaguzi
Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) – Mstaafu kwa kushirikiana na
aliyekuwa Mtendaji Mkuu
wa Shirika la
Maendeleo la Mafuta
nchini ,(TPDC),Yonna Killagane waliona hitaji
la kuanzisha Taasisi-Fikra ya Usimamizi isiyo ya kiserikali
itakayomilikiwa na wananchi
wenyewe ambayo itahusika
na uchambuzi wa mfumo na masuala ya uwajibikaji na utawala
bora nchini.
Amesema wameandaa mkutano wa
kwanza wa kimataifa utakaohusu
uwajibikaji katika sekta
ya gesi asilia
na mafuta kwa
kuzingatia umuhimu wa sekta hii
kwenye maendeleo ya nchi utakaofanyika kuanzia Aprili 11 hadi 12 Aprili 2016
katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwl. Julius Kambarage Nyerere
No comments:
Post a Comment