RAIS DKT. MAGUFULI AKAGUA NA KUWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA UJENZI WA KITUO CHA KUFUA UMEME CHA KINYEREZI II JIJINI DAR.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwa na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida, Waziri wa Nishati na
Madini Profesa Sospeter Muhongo, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa
wa Dar es Salaam CCM, Ramadhan Madabida, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini Dkt. Juliana Palangyo wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi
wa Ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji
la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza
maelezo kutoka Meneja wa Kituo cha kufua umeme cha Kinyerezi I Mhandisi
John Mageni kuhusu utendaji kazi wa kituo hicho.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo, Balozi wa Japan
Nchini Masaharu Yoshida, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ,
Mama Janeth Magufuli wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa
TANESCO mara baada ya kuzindua rasmi ujenzi wa Kituo cha Kufua umeme
cha Kinyerezi II nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza kwa makini mama mmoja alijitokeza kumpongeza kutokana na
utendaji kazi mzuri wa Serikali yake ya awamu ya tano mara baada ya
uzinduzi rasmi ujenzi wa wa Kituo cha Kufua umeme cha Kinyerezi II nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment