Header Ads

NAIBU WAZIRI ANASTAZIA WAMBURA AFUNGUA MAONYESHO YA SABA YA BIDHAA ZA HARUSI

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Anastazia Wambura akimkabidhi Cheti cha ushiriki Bw.Erasto Mike wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya saba ya bidhaa za harusi leo jijini Dar es Salaam.
Mhe. Anastazia Wambura Naibu waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo akiangalia bidhaa kutoka kwa mjasiriamali Bi Helen-Lukundo Chonjo( Kulia) wakati alipokuwa akifungua maonyesho ya saba ya bidhaa za Harusi.Katikati ni mbunifu wa mavazi Bw. Mustafa Asanali.
Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura akipokea maelekezo kuhusu jarida la Bidhaa za Harusi kutoka kwa mbunifu Mustafa Asanali kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Sanaa Bi Leah Kihimbi.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Anastazia Wambura akisikiliza ufafanuzi kuhusu bidhaa za harusi zinazotengenezwa hapa nchini kutoka kwa Bi Dianna Kaijage wakati alipofungua maonyesho ya saba ya bidhaa hizo leo jijini Dar es Salaam.
Bi Sakina Kubino akimuonyesha Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Anastazia Wambura baadhi ya urembo unaovaliwa katika Sherehe za harusi wakati alipofungua maonyesho ya bidhaa hizo leo jijini Dar es Salaam.
Mbunifu wa mavazi Bw. Mustafa Asanali akimkaribisha Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo katika maonyesho ya saba ya bidhaa za harusi yanayofanika katika ukumbi wa St Peters jijini Dar es Salaam

No comments:

Powered by Blogger.