MKUU WA MKOA WA KIGOMA AWATAKA WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZI KUTAJA KIIASI CHA FEDHA KILICHOTUMIKA KUWALIPA WATUMISHI HEWA 169
Mkuu
wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga akitoa
taarifa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu ya watumishi hewa
169 waliopo katika halmashauri za Mkoa wa Kigoma.
Na Editha Karlo, wa blog ya jamii Kigoma.
MKUU
wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali Emanuel Maganga amewataka wakuu wa
Wilaya na wakurugenzi wote waliopo katika halmashauri zote kutaja kiasi
cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169 kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Akiongea
na waandishi wa habari Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia jenerali Emanuel
Maganga alisema kuwa kufuatia agizo la Muheshimwa Rais juu ya kufanya
uhakiki wa watumishi katika halmashauri zote ili kuwabaini watumishi
hewa wanaolipwa mishahara kinyume na utaratibu za utumishi.
Alisema
katika hao watumishi hewa 169 waliowabaini wapo ambao walishafukuzwa
kazi, wapo ambao wameshafariki na wengine hawana sifa za kuwa watumishi
wa umma.
Maganga
alisema kuwa suala la kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi ambao hauwezi
kuvumilika na wizi wa kuibia wanyonge hauwezi kuvumilika.
"Hakuna
anayeweza kuvumilia wizi wa waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi ya
watumishi wasiowaaminifu, wale wote watakaobainika wajiandae kwani
hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao"Alisema Maganga.
Alisema
kuwa fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwaajili ya
mishahara zinatakiwa kurudi zote pia wakurugenzi wawafute watumishi hao
hewa kwenye orodha ya malipo.
Mkuu huyo wa Mkoa alisema kuwa sasa hivi katika serekali hii ya awamu ya tano hakuna kufanya kazi kwa mazowea.
Alizitaja
halmashauri zenye watumishi hewa kuwa ni halmashauri ya kasulu
watumishi 78,halmashauri ya Kigoma 23,Manispaa ya Kigoma Ujiji
29,halmashauri ya Buhigwe 11,Uvinza 19,kibondo 5,ofisi ya Mkuu wa Mkoa 4
na halmashauri ya Kakonko hakuna mtumishi hewa.
No comments:
Post a Comment