UKAGUZI WA SERIKALI KUU,IDARA,TAASISI MASHIRIKA YA UMMA HAUJAKAMILIKA -CAG.
Naibu
Mkazi Mkuu wa Hesabu za Serikali , Idara na Mashirika ya Umma,
Benjamin Mashauri, akizungumza na waandishi wa habari (hawako pichani)
kuhusu ukaguzi kwa Serikali Kuu, Mashirika ya mma na Serikali za Mitaa
kwa mwaka 2014/15, Dar es Salaam, jana. Kulia ni Sarah Reubeni,
Msemaji wa ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
OFISI
ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),imesema kuwa
ukaguzi wa mwaka 2014/2015 kwa serikali kuu haujakamilika hivyo kutumia
rasimu hiyo ni makosa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Naibu Mkaguzi wa
Mashirika ya Umma, Benjamin Mashauri amesema kuwa taarifa ya mkaguzi
inakamilika ni baada ya kuiwasilisha kwa Rais kwa mujibu wa katiba
inatakiwa iwasilishwe mwishoni mwa machi mwaka huu.
Mashauri
amesema kuwa taarifa zinatolewa baadhi ya vyombo vya habari na kunukuu
ripoti ya CAG kwa mwaka wa fedha 2014/2015 ni batili kutokana na
taarifa hiyo haijakamilika na wananchi wanatakiwa kupuuza taarifa hizo.
Amesema
rasmu hiyo inayotumika baadhi vyombo vya habari wakati taarifa hiyo
haijakamilika na kukamilika kwake ni mara ya kuwasilishwa kwa Rais na
kupeleka katika bunge na hapo inakuwa imekamilika kwa kutumia kwa ajili
ya wananchi juu ya fedha ya umma ilivyotumika.
"Kuendelea
kutumia rasmu hiyo wakati haijakamilika ni kupotosha watanzania na
kukiuka maadili ya kiutendaji na taaluma yake kwa kuwapa taarifa zisizo
na uhakika"amesema Mashauri.
Amesema
kuwa ofisi hiyo itaendelea na kutekeleza majukumu yake yote kwa
kuzingatia misingi na uwazi na uwajibikaji usiokiuka taratibu za
kisheria katika kukusanya na kutumia rasilimali za umma.
No comments:
Post a Comment