TOP 10 YA MAJESHI HATARI DUNIANI KWA SASA NA BAJETI ZAKE!
Jeshi
ni sehemu muhimu ya nchi na usalama wake. Kila mwaka nchi hutenga bajeti
kwa ajili ya kuimarisha majeshi yake. Nchi nyingi duniani huchukua
tahadhari za kiusalama kwa kuimarisha majeshi yake kulinganisha na nchi
nyingine zinavyofanya. Nchi hizo hufanya hivyo kwa kumiliki idadi kubwa
ya wanajeshi, kuboresha teknolojia ya kijeshi, kutoa mafunzo na
kutengeneza propaganda za kidiplomasia ili kuwaogopesha maadui wao wa
kiusalama.
Ngoja tuangalie majeshi kumi (Top 10) hatari duniani kwa sasa na bajeti
zake;
Wanajeshi wa Japani.
10:
JAPAN
Japan ilikuwa moja ya nchi vinara katika Vita ya Pili ya Dunia (WW2)
iliyomalizika mwaka 1945. Cha kufurahisha, baada ya vita hiyo, Japan
iliingia kwenye mkataba wa amani na kukubaliana kuwa na jeshi la kawaida
lakini kufuatia kukua kwa Jeshi la China ndipo ikaanza kupanua tena
jeshi lake ikiweka ngome za kijeshi kwenye visiwa vyake.
Bajeti ya Jeshi la Japan imekuwa ikiongezeka kila mwaka hadi kufikia
Dola za Kimarekani bilioni 49.
Jeshi hilo lina zaidi ya wanajeshi 247,000 waliopo kazini na zaidi
60,000 wa akiba. Lina ndege za kivita zipatazo 1,595 na meli 131.
Wanajeshi wa Korea Kusini wakifanya mazoezi.
9:
KOREA KUSINI
Korea Kusini wanashirikiana mpaka na Korea Kaskazini ambao nao wapo
vizuri kijeshi. Ili kukabiliana na majeshi makubwa ya China and Japan,
Korea Kusini imekuwa ikiongeza bajeti ya jeshi lake hadi kufikia dola
bilioni 34. Lina wanajeshi waliopo kazini 640,000 na wengine wa akiba
2,900,000. Lina ndege kubwa za kivita 1,393 na meli za kijeshi 166.
Wanajeshi wa Uturuki.
8:
UTURUKI
Labda ni kwa sababu ya kushirikiana kupambana na kundi korofi la kigaidi
la Islamic State linalotishia amani duniani ndiyo maana ni kubwa na
linaogopeka zaidi. Limeongeza bajeti yake kwa 10% hadi kufikia dola
bilioni 18.
Lina wanajeshi wapatao 660,000 walioko kazini na wa akiba. Pia lina
ndege za kivita 1,000 na silaha za nchi kavu 16,000 likiwa lina
ushirikiano mkubwa na lile la Marekani.
Wanajeshi wa Ujerumani.
7:
UJERUMANI
Miongoni mwa nchi zenye majeshi hatari duniani ni Ujerumani. Linatengewa
bajeti ya dola bilioni 45, japokuwa linaonekana kushuka katika miaka ya
hivi karibuni labda kwa sababu kizazi cha sasa nchini humo hakipendi
mambo ya vita na watu wengi wanaogopa kujiunga na jeshi hilo.
Lina wanajeshi 183,000 walioko kazini na 145,000 wa akiba likiwa na
ndege za kivita 710 na silaha za nchi kavu zaidi ya 5,000.
Wanajeshi wa Ufaransa.
6:
UFARANSA
Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imepunguza bajeti ya jeshi lake
hilo kwa 10%. Bajeti yake inafikia dola bilioni 43 kwa mwaka. Lina
wanajeshi 220,000 waliopo kazini na 500,000 wa akiba. Pia lina ndege za
kivita 1,000 na vifaa vya nchi kavu 9,000.
Waajeshi wa Uingereza.
5: UINGEREZA
Uingereza ni miongoni mwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) ambao wapo kwenye mkakata wa kupunguza wanajeshi wake kwa 20%.
Bajeti ya jeshi lake hatari ni dola bilioni 54 kwa mwaka likiwa na wanajeshi 205,000, ndege za kivita 908 na meli 66.
Wananchi wa India wakiwa katika mazoezi.
4:
INDIA
Jeshi lake lina jumla ya ‘wajeda’ milioni 3.5, wakiwemo milioni 1.325
waliopo kazini na wengine ni wa akiba. Lina magari ya kivita 16,000 na
ndege 1,785 pamoja na silaha za nyuklia. Bajeti yake ni dola bilioni 46.
Wanajeshi wa China.
3:
CHINA
Bajeti ya Jeshi la China inafikia dola bilioni 126 likiwa na wanajeshi
milioni 2.285 waliopo kazini na milioni 2.3 wa akiba. Ni moja ya majeshi
makubwa kwa sasa duniani likiwa katika Tatu Bora.
Lina vifaa vya kivita vya nchi kavu 25,000 na ndege 2,800. Pia lina
silaha za nyuklia 300.
Wanajeshi wa Urusi.
2:
URUSI
Bajeti ya jeshi hatari la Urusi ni dola bilioni 76.6 ambayo inatarajiwa
kuongezwa kwa 44%.
Tangu alipoichukua Urusi, Rais Vladimir Putin mwaka 2000, nchi hiyo
imekuwa moto wa kuotea mbali katika masuala ya kijeshi. Lina wanajeshi
766,000 waliopo kazini na milioni 2.5 wa akiba. Urusi inaongoza kwa
silaha za kivita zikiwemo za nyuklia zipatazo 8,500
Wanajeshi wa Marekani.\
1:
MAREKANI
Jeshi kinara la Marekani linatengewa bajeti ya dola bilioni 612.5.
Hakuna jeshi lenye bajeti kama hiyo duniani. Lina wanajeshi milioni 1.4
waliopo kazini na 800,000 wa akiba. Hawa jamaa ni wabaya kwa ndege, meli
na manowari za kivita. Pia lina silaha za nyuklia 7,500. Kama ulikuwa
hujui ndilo jeshi namba moja duniani tangu Vita ya Pili ya Dunia
iliyomalizika mwaka 1945.
Nchi kama Urusi na China zinangoja sana kwa jeshi la Marekani kutokana
na kuwa na mbinu na teknolojia ya hali ya juu ya kijeshi.
NB: Data kama hizi ni vigumu kuzipata kwa baadhi ya nchi za Afrika.
Imeandaliwa na Sifael Paul kwa msaada wa mtandao.
No comments:
Post a Comment