Header Ads

JK AONGOZA SHEREHE ZA MAADHIMISHO YA MIAKA 39 YA CCM MKOANI SINGIDA

 Mwenyekiti wa CCM,Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt  Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wakazi wa Singida na vitongoji vyake ndani ya uwanja wa Namfua,wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa CCM,mkoani Singida.Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi Mbalimbali wa Kitaifa,akiwemo Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli,Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan,Waziri Mkuu,Mh.Kasim Majaliwa.
 Baadhi ya Wananchi na wafuasi wa chama cha Mapinduzi (CCM) wakisikiliza hotuba iliyokuwa ikisomwa na Mwenyeki wa chama hicho,Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 39 tangu kuanzishwa kwake ndani ya uwanja wa Namfua leo mchana mkoani Singida.
 Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi waliokuwa wamekusanyika kwenye uwanja wa Namfua kushuhudia sherehe za maadhimisho ya miaka 39 ya CCM mapema leo mchana mkoani Singida
 Rais John Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
 Rais John Magufuli akimpongeza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwa hotuba yake wakati wa maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa CCM, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa CCM Namfua, mjini Singida leo.
 Sehemu ya umati wa wananchi wakiwa katika maadhimisho hayo.
 Mwenyekiti wa CCM Dkt Jakaya Kikwete akiwa ameongozana na Rais Dkt John Pombe Magufuli wakishuka jukwaani kwa pamoja mara baada kuhitimisha shughuli za maadhimisho ya miaka 39 ya chama hicho mkoani Singida,nyuma ni Makamu wa Rais Mama Samia Suluh Hassan.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi madawati 1000 kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Paraseko Kone kwenye maadhimisho ya kutimia miaka 39 ya CCM yaliyoadhimishwa leo Februari 06,2016 katika Uwanja wa Namfua Mkoani Singida. Kushoto Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan katikati Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiagana na Rais Dkt John Pombe Magufuli.


No comments:

Powered by Blogger.