Airtel Tanzania yapanga upya muundo wa utendaji kuboresha huduma
Dar es Salaam Tanzania Februari 8 2016, Kampuni
ya Simu za mkononi nchini Airtel Tanzania, leo imetangaza mkakati wake
wa kuboresha muundo katika nafasi zote za utendaji kuwa bora zaidi na
kuweka idadi sahihi ili viwango vya kiutendaji kuimarika na hatimae
dhamira yake ya pkibiashara ya kutoa huduma na bidhaa bora za
kimawasiliano nchini Tanzania kufikiwa.
Taarifa
iliyotolewa leo na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Bi, Beatrice
Singano alisema “ Mkakati huu wa kuboresha upya mfumo wa utendaji wa
kampuni yetu ni sambamba kabisa na mfumo wetu wa maboresho uliowekwa na
kampuni yetu ambao tunaamini baada ya muda mfupi utakuwa na mafanikio
makubwa kwa wadau wote wakiwemo wafanyakazi na wateja wetu
tunaowahudumia”
Singano
akifafanua alisema “Maboresha haya tunayofanya yatawahusisha takribani
wafanyakazi 55 kwa nafasi zao za utendandaji kutokuwepo au kuhamishiwa
kwa wadau watakao toa huduma kwa kampuni yetu, mfumo ujulikanao kama
“outsource model”, watoa huduma tutakaowapa jukumu la kusimamia baadhi
ya huduma zetu”
Airtel
tangu kuanza kwa mkakati huu wa maboresho yake ya kiutendaji kwaajili
ya kutimiza malengo ya kibiashara imejizatiti kwa kuweka miundombinu
madhubuti kwa kuingia mikataba ya kiutendaji.
“Vilevile
kama njia ya kushirikiana na wale watakao guswa na zoezi hili la
marekebisho ya mfumo huu kipindi hiki cha mpito, Airtel tayari imeingia
mkataba na kampuni inayohusiana na huduma za rasilimaliwatu ili kutoa
mafunzo na ushauri wa kutosha ya jinsi ya kutafuta na kuzipokea nafasi
zingine zinazojitokeza, Malipo ya huduma hii kwa wote watakaohitaji
yamegaramiwa na Airtel” alimaliza kwa kusema Bi, Singano .
No comments:
Post a Comment