Header Ads

WAZIRI KITWANGA AKUTANA NA VIONGOZI WA WILAYA YA MISUNGWI, ACHANGIA MIRADI YA MAENDELEO.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza mara baada ya kupokelewa wilayani hapo. Waziri Kitwanga aliwataka viongozi hao kuongeza nguvu kubwa ya kukusanya kodi kwa wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa na si kuwasumbua wafanyabiashara wadogowadogo. Pia aliwataka viongozi hao wahakikishe hakuna mwanafunzi atakayekaa chini darasani ifikapo mwakani.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Maabara katika Shule ya Sekondari Aimee Milembe wilayani humo. 
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akiwauliza maswali viongozi wa Kata ya Mabuki wilayani Misungwi wakati alipokuwa anakagua ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kijiji cha Mhungwe katika kata hiyo. Waziri Kitwanga alichanga milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa Kituo hicho cha afya. Wapili kulia ni Diwani wa Kata hiyo, Nicodemus Ihano, na wapili kushoto ni Mtendaji wa Kata hiyo, Angelina Nyanda.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) akiangalia ufa katika moja ya madarasa ya Shule ya Msingi Lubuga iliyopo Kata ya Mabuki wilayani Misungwi. Waziri Kitwanga aliagiza darasa hilo livunjwe na ameahidi kuchangia matofali pamoja na mifuko ya saruji.

No comments:

Powered by Blogger.