CLOUDS TV YAINGIA RASMI KWENYE KING’AMUZI CHA DStv “CHANELI 294”
MultiChoice Africa inapenda kuwatangazia wateja wake na watanzania kwa ujumla kuwa Clouds TV sasa imeingia rasmi kwenye DStv.
Kile
kilio cha muda mrefu cha watazamaji na wapenzi wa Clouds TV juu ya
Clouds TV kukosekana kwenye king'amuzi cha DSTV kimesikika na sasa
Clouds TV imeingia rasmi ndani ya DStv.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Meneja Uendeshaji MultiChoice Tanzania, Ndugu
Ronald Baraka Shelukindo, amesema baada ya mazungumzo ya muda mrefu
kati ya Clouds TV na Multichoice Africa kuhusu Clouds TV kuingia katika
king'amuzi cha DStv, MultiChoice Africa na Clouds TV wamefikia muafaka
ambapo watazamaji na wapenzi wa Clouds TV wenye ving'amuzi vya DStv
watapata uhondo wa Clouds TV ndani ya DStv.
Akiongezea,
Meneja Mauzo wa MultiChoice Tanzania , Ndugu Salum Salum ameelezea
furaha ya kampuni yao na akasema, wakati mwingine walikuwa wanashindwa
kufikia lengo la kupata wateja wengi zaidi kutokana na kukosekana kwa
Clouds TV “hivyo kuanzia sasa, tuna imani kuwa idadi ya wateja
itaongezeka maradufu!”.
Clouds
TV itaanza kupatikana rasmi ndani ya DStv tarehe 14 Januari 2015,
kwenye Chaneli 294, katika vifurushi vyake vyote ikiwemo; Premium,
Compact Plus, Compact , Family na kifurushi cha DStv Bomba.
No comments:
Post a Comment