TANZAONE: MMEA WA ‘LOZERA’ HAUFAI KWA MATUMIZI YA BINADAMU
Tabibu Gonzaga Marwa akiangalia baadhi ya mkopo ya Dawa jijini Dar es Salaam leo
TAASISI
isiyo ya Kiserikali ya Tanzaone Herbal Clinic chini ya mradi wake wa
‘Tanzaone’ hatimaye imethibitisha pasipo shaka kuwa mmea ujulikanao kama
Lozera na bidhaa zitokanazo na mmea huo hazifai kwa matumizi ya
binadamu na wanyama.
Akizungumza
na waandishi wa habari, sanjari na kuonyesha majibu ya vipimo vya
kitaalamu kutoka Wakala wa Maabara ya Ofisi ya Mkemia Mkuu wa serikali
kupitia utafiti uliofanywa chini ya mradi huo, Mratibu wa mradi.
Tabibu
Gonzaga Marwa, amesema matokeo ya uchunguzi wa sampuli za mmea huo
yameonesha una ukuvi yaani ‘fangasi’ aina ya Aspergillus ambao hutoa
sumu ya Aflatoxin ambayo huweza kusababisha saratani ya maini.
Aidha,
Tabibu Marwa ameiomba serikali kupitia Wizara ya Afya, na Mamlaka ya
Chakula na Dawa TFDA, kuhakikisha wanachukua hatua za haraka kunusuru
afya za walaji, sambamba na kushauri wadau wa tiba asili nchini kufanya
utafiti wa kina wa dawa za mitishamba na bidhaa zake kabla ya kumfikia
mlaji.
Hati
ya uchunguzi ya Mradi huo, namba 241/2013, uliopewa jina la ‘Tanzaone
Red Tea Juice’ na kudumu kwa miaka mitatu 2010/2013, kwa kushirikisha
watuamiaji wakubwa wa Lozera zaidi ya 250 nchini kote, ilichunguzwa,
kuidhinishwa na kuthibitishwa na Mkemia Mkuu wa Serikali
No comments:
Post a Comment