MSD YAPELEKA MOI VIFAA VYENYE THAMANI YA SH.MILIONI 251 ZILIZOKUWA ZITUMIKE KUJIPONGEZA WABUNGE
Magari
ya Bohari ya Dawa (MSD), yakishusha vifaa tiba Taasisi ya Moi kufuatia
agizo la Rais Dk.John Magufuli kulitaka Bunge kutumia sh.milioni 15 kwa
ajili ya kujipongeza na fedha zilizobaki kuzipeleka katika Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili kukabiliana na uhaba wa vifaa tiba na magodoro.
Na Dotto Mwaibale
…………………………………………………………………………
BOHARI
ya Dawa (MSD) imeanza kupeleka Vifaa Tiba kwenye Taasisi ya Mifupa ya
Muhimbili (MOI), Vifaa ambavyo vimenunuliwa na Ofisi ya Bunge kwa agizo
alilotoa Rais Dk. John Magufuli.
Vifaa
hivyo vilianza kupelekwa juzi katika Taasisi hiyo ili kukabiliana na
uhaba alioubaini Rais Magufuli baada ya kufanya ziara ya kushitukiza
katika mapema mwezi huu.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akizungumzia kuhusu
vifaa hivyo jijini Dar es Salaam juzi wakati wa usambazaji alisema
hivyo vyenye gharama ya sh.milioni .251 ni pamoja na vitanda 300,
magodoro 300, viti vya kusukuma (Wheel Chairs) 30, vitanda vya kubebea
wagonjwa (Stretchers) 30, mashuka 1,695 na mablanketi 400.
Alisema MSD ilianza kupeleka Vifaa hivyo MOI mwishoni mwa wiki na kuwa itaendelea kutoa vifaa hadi wiki hii inayoanza leo.
Fedha
hizo zilizotumika kununulia vifaa hivyo zilitokana na agizo la Rais
Dk.John Magufuli alilolitoa wakati akilihutubia bunge mjini Dodoma
mwishoni mwa wiki ambapo alilitaka bunge kutumia sh.milioni 15 tu kwa
ajili ya kujipongeza na kiasi hicho kilichobaki kitumike kununulia vifaa
hivyo.
No comments:
Post a Comment