BENKI YA POSTA YABORESHA ZAIDIN HUDUMA ZAKE, MTEJA ATATOA MAONI BILA KUANDIKA KWENYE KARATASI, NI "KUBOVYA TU" KWENYE MASHINEAKATHE
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania, TPB, Sabasaba Moshingi(wapili
kulia), akihudumia wateja kwenye tawi la benki hiyo Kijitonyama jijini
Dar es Salaam, leo Ijumaa Oktoba 16, 2015, kwenye kilele cha maadhimisho
ya wiki ya huduma kwa wateja ya benki hiyo. (Picha na K-VIS
MEDIA/Khalfan Said)
NA K-VIS MEDIA
KATIKA
kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake hapa nchini, Benki ya
Posta Tanzania, imeweka mashine maalum ambayo wateja wa benki hiyo
wanaofika kupatiwa huduma watatoa maoni yao juu ya huduma wazipatazo kwa
kubonyeza vitufe vinavyoelekeza nini maoni yake juu ya huduma
aliyoipata.
Akizungumza
na waandishi wa habari wakati wa kilele cha maadhimisho ya wiki ya
huduma kwa wateja ya benki hiyo, kwenye tawi lake la Kijitonyama jijini
Dar es Salaam, Oktoba 16, 2015, Aisa Mtendaji Mkuu wa benki hiyo,
Sabasaba Moshingi alisema, benki yake imelenga kutoa huduma zilizo bora
na za kisasa ili kurahisisha utendaji wake wa kazi.
Moshingi
ambaye aliongoza maafisa wa benki hyo kutoka makao makuu kwa kutoa
huduma kwa wateja, kuwasikiliza na kuwasaidia namna ya kujaza fomu na
kutoa pesa, alisema,hatua ya yeye kuongoza maafisa wake kutoa huduma, ni
kuwaonyesha wateja kuwa benki yao inawajali.
“Ili
kufanikisha lengo hili benki imeanzisha matumizi ya mashine za kisasa
zitakazomuwezesha mteja kutoa maoni ya jinsi gani anafurahia au
kutofurahia huduma zetu bila kuhitaji kuandika kwenye karatas, mteja
atabofya kitufe ili kupata maoni yake, nasi tutayafanyia kazi maoni yake
haraka iwezekanavyo.”i.” Alisema Moshingi.
Alisema
matumizi ya mashine hizo yataboresha utoaji huduma za kibenki, na hivi
sasa mipango ya kuziweka kwenye kila tawi inaendelea.
Moshingi akimuelekeza mteja namna ya kujaza fomu za kuweka pesa
Afisa wa operesheni wa TPB tawi la Kijitonyama, Agatha Ngoile, (kushoto), akimuhudumia mteja
No comments:
Post a Comment