CCM ZANZIBAR WAANZA MCHAKATO WA KUTOA FOMU KWA WAGOMBEA WA UBUNGE

Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikabidhiwa Fomu na
Katibu wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B “ Bibi Subira Mohammed kuomba
ridhaa kwa CCM kugombea Uwakilishi Jimbo Jipya la Mahonda.

Katibu
wa Chama cha Mapinduzi {CCM} Wilaya ya Kaskazini “B “ Bibi Subira
Mohammed akimpatia maelezo Balozi Seif mara baada ya kumkabidhi Fomu kwa
ajili ya kuomba ridhaa ya kugombea Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Jimbo la Mahonda hapo Ofisi ya CCM Wilaya hiyo Mahonda.

Balozi
Seif akimkabidhi shilingi Laki 300,000/- Katibu wa CCM Wilaya ya
Kaskazini “B” Bibi Subira Mohammed ikiwa ni ada ya Fomu alizopewa kwa
ajili ya kuomba kuteuliwa kugombea Uwakilishi Jimbo la Mahonda kwa
Tiketi ya CCM katika uchaguzi Mkuu ujao.
Picha na –OMPR – ZNZ.
WAKATI
Chama cha Mapinduzi kimeanza zoezi la kutoa fomu kwa ajili ya Wanachama
wake wenye nia kutaka kugombea nafasi za Uwakilishi, Ubunge, Udiwani
na Viti Maalum vya wanawake, wazazi na Vijana mapema leo asubuhi baadhi
ya wanachama wa chama hicho tayari wameshajitokeza kuchukuwa fomu hizo.
Zoezi
hilo limekuwa likiendeshwa kwenye Ofisi zote za Chama cha Mapinduzi za
Wilaya hapa Nchini na linatarajiwa kuendelea hadi Saa Nane Mchana ya
Tarehe 19 mwezi huu wa Julai.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali ni miongoni mwa Wanachama
hao wa CCM waliojitokeza kuchukuwa fomu hizo akijiandaa kuomba kuwania
nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar katika Jimbo Jipya la
Mahonda ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.
Balozi
Seif Ali Iddi ni Mmoja miongoni mwa Wanachama wanane wa CCM
waliojitokeza hadi hivi sasa wenye nia ya kutaka kugombea nafasi ya
Uwakilishi katika Majimbo mbali mbali ya Wilaya ya Kaskazini “B”ambao
tayari wameshachukuwa Fomu hizo.
Katibu
wa CCM Wilaya ya Kaskazini “B” Bibi Subira Mohammed akimkabidhi Fomu
hizo hapo Ofisini kwake Mahonda alimueleza Balozi Seif kwamba yuko huru
kujeresha fomu hizo wakati wowote amalizapo kujaza kuanzia leo hadi
Tarehe 19 Julai majira ya Mchana.
Bibi
Subira alisema Mwanachama mwenye nia ya kutaka kugombea nafasi hizo
anawajibika kuzilipia Fomu hizo kwa kiwango cha shilingi Laki 300,000/-
kama ada rasmi iliyowekwa na Chama pamoja na mwanachama huyo kuchangia
chama kwa kadri ya kiwango anachokimudu.
Hadi
sasa tayari wanachama wa Chama cha Mapinduzi wapatao kumi
wameshajitokeza kuchukua Fomu za kuomba kugombea nafasi za Ubunge na
Wanachama Wanne kwa Nafasi za Udiwani Ndani ya Wilaya ya Kaskazini “B”.
Katika
safari hiyo ya uchukuaji Fomu za kutaka kugombea nafasi mbali mbali za
Uongozi kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwezi Oktoba Mwaka huu wa 2015
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliambatana na wake zake
wote wawili Mama Pili Seif Iddi na Mama Asha Suleiman Iddi na
kushuhudiwa na baadhi ya Viongozi wa CCM Wilaya na Jimbo la Kitope.
No comments:
Post a Comment