WAHITIMU KIDATO CHA SITA JANGWANI WAASWA KUTUMIA ELIMU KAMA SILAHA YA UKOMBOZI.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola na akisalimiana na
baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwishoni mwa wiki wakati alipokuwa
mgeni rasmi katika wa mahafali hayo shuleni Jangwani sekondari iliyopo
manispaa ya Ilala Jijini Dare s salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola (wa katikati) na
baadhi wa viongozi wa shule wakielekea eneo la mahafali ya kidato cha
sita ya shule ya sekondari Jangwani yalifanyika mwishoni mwa wiki ambapo
Mkurgenzi huyo alikuwa mgeni rasmi. Wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Shule
ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga.
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu wa Shule ya sekondari Jangwani wakielekea eneo la mahafali yao.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola akitoa hotuba yake
wakati wa mahafali ya kidato cha sita shule ya sekondari Jangwani
mwishoni mwa wiki na kuwaasa watumie nidhamu bora ambayo itawasaidia
kufikia malengo yao waliyojiwekea maishani mwao. Kushoto ni Mkuu wa
Shule ya sekondari Jangwani Geraldine Mwanisenga.
Mwanafunzi
aliyepata vyeti mbalimbali vya taaluma takribani saba kwa kufanya
vizuri katika masomo ya Kemia, Biyolojia, Fizikia, Hesabu, cheti cha
kuwa mwanafunzi bora katika masomo, uongozi, uongozi bora pamoja na
zawadi Rosemary Mushi akipongezwa na Mgeni Rasmi na Mkurugenzi Mtendaji
wa Tausi Dreams Foundation Tausi Likokola na kukabidhiwa vyeti vyake
wakati wa mahafali ya kidato cha sita yalifanyika shule ya sekondari
Jangwani mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment