BODI YA TAFF TAIFA YAMNG’OA KATIBU BISHOP HILUKA UONGOZI
:- Kwa kusuka mipango ya kumng’oa Rais Mwakifwamba
NI kikao kilichochukua zaidi ya saa nane kujadili agenda kadhaa
lakini iliyoonyesha kuwa ni hatari na kuchukua muda wa wajumbe ilikuwa ni
mikakati inayosemekana kusukwa na katibu Bishop Hiluka kutaka kumng’oa rais wa
shirikisho la Filamu Tanzania Simon Mwakifwamba, hatimaye Bodi kwa kupiga kura
ikafikia muafaka kuwa katibu aachie ngazi na Rais aendelee na uongozi.
Awali Bishop alikataa kujiudhuru kwa maelezo kuwa mwenye mamlaka
ya kumuwajibisha ni Bodi ya Taff na si Rais wala makamu wake, jambo lilozua
mjadala mkubwa baada ya Mwakifwamba kusema kuwa wajumbe wa Bodi haikuwa rahisi
kumtambua yeye bila ya yeye kumtambulisha na wajumbe wakampitisha.
Uhasama uliopo inasemekana kuwa Katibu amekuwa akitoa siri za
shirikisho kwa wapinzani na wasilitakia mema shirikisho, jambo ambalo
lilimshitusha Rais na kuanza kufanya kazi kwa taadhali huku akimwangalia katibu
wake, baada ya kufikia hatua hiyo ndipo Bodi ilipokutana leo ikiwa na nia ya
kujadili baadhi ya mikataba ya Taff na wadau wanaotaka kufanya nao kazi.
Kikao kilibadili mwelekeo baada ya katibu kuleta agenda ya
mpasuko ndani Taff ambapo Rais alipinga kuwa agenda hiyo haikuwepo katika
agenda zilizopo jambo lililoonyesha kuwa watu hawa hawana mawasiliano pamoja
kuwa ni watu wanaotegemea kiutendaji na kuonyesha hofu kubwa hasa pale
Mwakifwamba aliposema kuwa hawezi kufanya kazi na Bishop.
FC iliongea na Katibu Bishop Hiluka baada ya kufikia maamuzi
yaliyofikiwa kupigiwa kura za kumtoa katika nafasi yake ya ukatibu wa Taff,
alisema kuwa kwake imekuwa nafuu kwani inampa nafasi ya kufanya kazi zake
nyingine zenye maslahi tofauti pale sehemu kubwa ya kujitolea na bado kuna majungu.
“Taff hali ni mbaya tusidanganyane, nimekuwa na mtafaruku mkubwa
sana na Mwakifwamba kiutawala kwani mwenzangu amekuwa
akitengeneza platform ndani ya Taff kunipaka matope na kuzusha mambo ambayo
hayana ukweli wala faida kwa tasnia ya filamu Tanzania,”anasema Bishop.
Bishop anasema kuwa aliomba kujiudhuru zaidi ya mara tatu lakini
bodi ya Taff imekuwa ikimzuia ikitaka asiondoke hadi asimamie
uchaguzi upite ndio wangeweza kuangalia njia ya kumpata katibu mwingine hivyo
hata alipoambiwa ajiudhuru alisema kuwa alishaomba mara nyingi sana kufanya
hivyo akazuiwa.
“Lakini leo wakaniambia nipumzike nimepata amani kwani nimekuwa
nikikosa hata pesa kwa ajili ya familia ya kwa ajili ya Taff, siku za hivi
karibuni nilipunguza kabisa kufika ofisini na kuangalia kazi zangu zinazonipa
riziki tena kwa amani,”anasema Bishop.
No comments:
Post a Comment