Zitto Kabwe: Tuhuma dhidi yangu zichunguzwe

----
Katika kujitetea mbele ya Baraza la Maadili kuhusu tuhuma dhidi yake za kugawiwa mgawo wa fedha kutoka akaunti ya Escrow, mbunge wa Sengerema Bwana William Ngeleja alisema kuwa ni kawaida wabunge kupewa misaada na wafanyabiashara na taasisi za umma. Katika Maelezo yake alirudia tuhuma za kipuuzi dhidi yangu zilizokwisha tolewa huko nyuma kwamba
1) nilipewa fedha na kampuni ya PAP na
2) nilipewa fedha na shirika la NSSF.
- Maelezo yangu kuhusu kazi za Kigoma AllStars/LEKADUTIGITE kwa NSSF na TANAPA.
- MAELEZO BINAFSI YA MHE. ZITTO ZUBERI KABWE DHIDI YA TUHUMA ZA RUSHWA HUSUSAN KUELEKEA KATIKA KUPITISHA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI
Tuhuma zote hizo nimewahi kuzitolea ufafanuzi na kukanusha kwani hazina msingi wowote na zilikuwa siasa za majitaka. Hata hivyo bado zimekuwa zikijirudia rudia kwa malengo maalumu wanayoyajua wanaotoa tuhuma hizo. Watuhumiwa wa ufisadi wa escrow hawajazoea kuona taasisi za maadili zikifanya kazi kwa namna ilivyo sasa na hivyo wanajaribu na watajaribu kubwabwaja na kuhangaika ikiwemo kutaka kila mtu aonekane ni mtuhumiwa kama wao. Ndio maana Bwana Ngeleja ametaja msururu wa watu wakiwemo wafanyabiashara kwamba huwapa fedha wabunge bila chembe ya ushahidi.
No comments:
Post a Comment