ZIARA YA KATIBU MKUU NDUGU KINANA NDANI YA JIMBO LA MOSHI VIJIJINI,LEO KUUNGURUMA JIMBO LA VUNJO MKOANI KILIMANJARO

Wakazi wa Kwa
Mangi kata ya Kibosho Kati wakimsikiliza Katibu Mkuu wa
CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokuwa akiwahutubia,Kinana aliwaeleza wananchi
hao kuwa kuna baadhi ya watu wamekuwa wakijipitisha pitisha kuomba
uongozi,hivyo amewaonya na kuwatahadharisha kutojipitisha
pitisha kugombea nafasi za uongozi kabla ya muda kuisha na kutangazwa.


Zaidi ya wanachama 335 wamejiunga na CCM kwenye mkutano
wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza
na mwanafunzi Elia PeterUlomi wa shule ya sekondari ya Somsom.

Jengo la chuo cha KVTC kama lionekavyo kwa nje,ambapo Katibu Mkuu wa CCM
Ndugu
Abdulrahman Kinana alitembelea

Shamba la Mpunga lililopo Mabogini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
wanafunzi
alipotembelea chuo cha KVTC-Kibosho Moshi vijijini.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki
kupanda mti wa kumbukumbu kwenye chuo cha Ufundi KVTC,Kibosho wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki uvunaji wa mpunga kweny
skimu ya umwagiliaji ya Lower Moshi.

Mbunge
wa Jimbo la Moshi Vijijini Ndugu Cyril Chami akihutubia wananchi wa
kijiji cha Chekereni kata ya Mabogeni. Kata ya Mabogeni ina vijiji 8 na
vyote vimeshinda kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Jimbo la Moshi Vijijini lina Kata 16 ,shule za sekondari zilizojengwa ni 29.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Chekereni kata ya Mabogini.
No comments:
Post a Comment